Wednesday 31 May 2017

Naomba mniache niondoke Leicester City – Mahrez

Kiungo wa klabu ya Leicester City ya nchini Uingereza Riyad Mahrez, amesema kuwa anataka kuondoka katika klabu hiyo.


Mchezaji wa klabu ya Leicester City ya nchini Uingereza Riyad Mahrez,

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26, alijiunga na klabu hiyo akitokea Le Havre ya nchini Ufaransa kwa ada ya uhamisho wa paundi 400,000 mwaka 2014,amesema alikubali kubaki klabuni hapo kwa msimu mwingine baada ya majadiliano mazuri na mwenyekiti walipoishangaza dunia kwa kuwa mabingwa wa ligi kuu nchini Uingereza EPL msimu uliopita.
Lakini kwa sasa amesema kuwa tayari ameweka wazi juu ya kuondoka kwake na anaomba klabu yake imruhusu kufanya hivyo.


Mchezaji wa klabu ya Leicester City ya nchini Uingereza Riyad Mahrez,

Mahrez ni mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa Uingereza mwaka 2016, amecheza mara 48 msimu huu akifunga magoli 10 na kutoa pasi saba zilizo changia kupatikana kwa magoli.
Leicester ilianza msimu wa ligi ya Uingereza vibaya na hatimaye kumaliza katika nafasi ya 12, lakini ikafanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya klabu bingwa barani Ulaya.