Mkali wa Aje kutoka Tanzania, Alikiba wiki hii alikuwa mmoja kati ya wasanii wakubwa wa Afrika waliofanya show katika tamasha kubwa la muziki ‘One Afrika Music Fest London’ lililofanyika nchini Uingereza.
Alikiba akiwa kwenye show hiyo
Show hiyo ilikuwa inaonyeshwa na TIDALXOneAfrica.
Kupitia mtandao wa label hiyo kubwa ya muziki Marekani, walipost picha ya Alikiba na kuandika ujumbe mzuri uliowafariji mashabiki wa muimbaji huyo.
“The unstoppable @OfficialAliKiba is live right now in #London: http://TIDAL.com/OneAfrica #TIDALXOneAfrica,” mtandao huyo uliandika wakiambatanisha na picha yake.
Baadhi ya wadau kwenye muziki wamedai hiyo ni hatua nzuri kwa muimbaji huyo kwa kuwa mtandao huyo unaangaliwa na watu wengi duniani.