Friday 27 January 2017

Roger Federer atinga fainali ya Australian Open 2017


Mcheza tenesi Roger Federer amefanikiwa kuingia hatua ya Fainali ya michuano ya Australian Open 2017 baada ya kumfunga Mswitzerland mwenzake Stan Wawrinka kwa seti 7-5 6-3 1-6 4-6 6-3 kwenye mchezo wa nusu fainali uliochukua muda saa 3 na dakika 5.





Federer,35, katika hatua hiyo anataraji kukutana na mshindi wa mchezo wa nusu fainali kati ya Rafael Nadal and Grigor Dimitrov.

Hii ni mara yake ya 28 kuingia fainali ya Grand Slam na endapo atashinda mchezo wa fainali jumapili hii, atakuwa amechukua ubingwa wa michuano hii mara 5 na itakuwa ni Grand Slam yake ya 18 kuchukua.