Friday 27 January 2017

Esha Buheti aweka wazi ishu ya ujamzito wake


Msanii wa filamu Esha Buheti amefunguka kwa kusema kuwa ni kweli ana mimba na sio kiki kama baadhi ya watu kwenye mitandao ya kijamii wanavyodai.




Muigizaji huyo ambaye aliibuka mshindi wa tuzo ya muigizaji bora wa ZIFF 2014, amedai kuna watu wanamtupia maneno machafu kuhusu mimba hiyo kitu ambacho hajapendezwa nacho.

Buheti amedai suala la kujifungua salama au sio salama ni mipango ya Mungu na sio binadamu.

“Jamani napokea maoni mengi mazuri na mabaya pia napokea matusi mengi na kejeli kwa wingi ila niwaambie ukweli mimi siigizi na sitafuti kiki yes me ni mjamzito na mungu akipenda nitajifungua salama muda ukifika,” Muigizaji huyo alitoa taarifa hiyo kupitia Instagram.

Aliongeza, “My point is jamani mimi na wewe maisha yetu yapo mikononi mwa mungu sio binadamu so kila linalotokea Mungu ndo mpangaji siezi acha kufanya jambo eti kisa kuna watu hawapendi watanidhuru, wakunidhuru ni Mungu msisahau jamani kuna mungu acheni kunyenyekea binadamu na kuwaogopa kiasi chakusahau hayo yote unatakiwa uyafanye kwa mungu wako. Please from now sitaki ushauri sababu at this age najua baya na zuri pia naamini mbele ya mungu nitakua salama. Naomba mniache kwa sasa plz plz yani kama ntapost kitu kitakuudhi pita kimya au nipe kufuli tuu sorry kwa ninao wakwaza . Narudia tena sorry kama kuna neno nimeongea limekukwaza ila naomba tuheshimiane na tusipangiane maisha,”