Tuesday 31 January 2017

KITENDO CHA CHUO KIKUU DAR ES SALAAM KUMFUKUZA MWANAFUNZI HUYU CHALANIWA KILA KONA

Alphonce Lusako kwaheri mpambanaji. Ulifukuzwa mwaka 2011 ukiwa mwaka wa 3, Kwa kutambua umuhimu wa elimu ukaamua kurudi chuo kuendelea na masomo yako kwa kuanza mwaka wa kwanza sheria 2016, lakini leo baada ya kutoka kwenye mtihani umekutana na barua ikikutaka uondoke chuo haraka kwa sababu kuwa ulisajiliwa kimakosa. Inauma sana lakini ndio gharama halisi ya harakati za kujitoa kwajili ya wengine. ALUTA CONTINUA

Nimesikitika kupata habari za Ndugu.Alphonce Lusako mwanafunzi wa UDSM aliyefukuzwa mara mbili chuoni hapo. Mwaka 2011 akiwa mwaka wa 3, (ambao ni mwaka wa mwisho wa masomo) alifukuzwa chuoni hapo kwa madai ya kuchochea mgomo. Kwa maelezo niliyopata ni kuwa hoja zake zilikua mbili. Mosi TCU inadahili wanafunzi hewa, pili Bodu ya mikopo inafanya ubadhirifu wa pesa za wanafunzi. Madai haya yakaonekana ni uchochezi na akafukuzwa chuo akiwa mwaka wa mwisho.
Akakaa mtaani miaka 6, bila kupewa barua ya kumuita tena chuoni. Mwaka jana akaamua kuomba tena nafasi ya kusoma kupitia TCU, wakampanga tena UDSM, kozi ya sheria. Akaamua kuanza mwaka wa kwanza. Sasa amesoma semester moja hatimaye jana akitoka kwenye chumba cha mtihani akapewa barua ya kufukuzwa tena chuoni. Sio kwamba amefanya kosa ila UDSM wamefukua makaburi ya mwaka 2011. Wamemfukuza tena wakidai walimdahili kimakosa alipoomba nafasi mara ya pili.
#MyTake:
1. Je UDSM walimfungia Lusako kusoma chuoni hapo milele?
2. Kwanini UDSM hawakumkataa alipoomba admission mara ya pili, badala yake wamemdahili na kusubiri apoteze muda kusoma semester moja ndio wamfukuze?
3. Hoja za Lusako kuhusu TCU na HESLB, zinafanana na hoja za Rais JPM kuhusu taasisi hizo. JPM amesema TCU ilikua ikidahili wanafunzi wasio na sifa na Bodi ilikua ikitoa mikopo kwa wanafunzi hewa. Hali hii ilipelekea JPM kufanya mabadiliko ya management kwenye taasisi hizo. Sasa ikiwa ndivyo, kwanini Lusako aendelee kuonekana na hatia?
Anyway, binafsi nimejisikia vby kuona taasisi za elimu zinatumia nguvu kubwa kulazimisha watu kuwa wajinga badala ya kupunguza ujinga. Taasisi za elimu zinapaswa kuwa na mazingira rafiki kwa kila mtu mwenye sifa na uwezo wa kusoma aweze kusoma.
Kama ni adhabu Lusako ameshatumikia vya kutosha. Kwanza kupoteza degree yake aliyokua amalize mwaka 2011 ni adhabu kali sana maana miaka yote mitatu alifanya kazi bure. Pili kukaa mtaani miaka 6 kwa kukosa fursa ya kusoma ni adhabu kubwa zaidi. Adhabu hizi mbili zilimtosha kabisa Lusako na kama ni kujifunza ameshajifunza vya kutosha.
Kwahiyo sioni kama kulikua na sababu ya kumfukuza tena mtu wa aina hii. Labda kama UDSM walidhamiria kumkomoa. Lakini kama ni adhabu iliyolenga kumfundisha nina hakika Lusako amejifunza vya kutosha, na UDSM haikua na sababu ya kumfukuza tena mara ya pili.
Tujenge taasisi za elimu zenye mazingira rafiki kwa wote. Zilenge kutatua changamoto za jamii, sio kuongeza changamoto kwa jamii. Nina imani Management ya UDSM ina fursa ya kupitia upya maamuzi yake kuhusu hatma ya kijana huyu na ikafanya maamuzi ya busara zaidi kuliko haya. Pole sana Lusako.!!