Saturday 1 April 2017

Waimbaji 10 waliyowahi kuambiwa hawajui kuimba lakini leo ni mastaa wa dunia



Mara nyingi watu wanaposhindwa na jambo hukata tamaa lakini kushindwa mara moja haimaanishi huwezi kufanikiwa jambo hilo ukijaribu tena na tena, leo nimekuletea list ya wanamzuiki kumi waliowahi kuambiwa hawajui kuimba na leo hii ni mastaa wakubwa duniani.

1: Beyonce

Akiwa na miaka 14 tu alipelekwa na baba yake Mathew Knowles arekodi nyimbo lakini producer alipomsikia Beyonce akiimba alimwambia hadhani kama kuimba ni kipaji chake lakini leo hii Beyonce ni miongoni mwa waimbaji wakubwa duniani akiwa na thamani ya zaidi ya dola za kimarekani Milioni 600 na kuuza zaidi ya rekodi milioni 34.


2: Shakira.

Shakira ni miongoni mwa waimbaji wenye mafanikio makubwa dunia akiwa na thamani ya zaidi ya dola milioni 220 na kuuza rekodi ya zaidi milioni 60 duniani kote lakini aliwahi kukataliwa kujiunga na kikundi cha kuimba kwaya kanisani kwao na mwalimu wake wa muziki kwa kumwambia ana sauti mbaya inayofanana na mbuzi.


3: Spice girls.


Spice girls ni moja ya kundi la muziki lililojipatia umaarufu mkubwa miaka ya 90 kwa kuuza zaidi ya rekodi milioni 85 duniani kote, lakini waliwahi kuambiwa na producer maarufu Simon Cowel kuwa hawatafika popote kimuziki na ana washauri waachane na muziki na kutafuta kazi nyingine.

4: One Direction.


One Direction ni kundi linalopendwa duniani na wamepata mafanikio makubwa kimuziki lakini mwanzoni mwa carrier yao waliposhiriki shindano la kutafuta vipaji la xfactor waliwahi kuambiwa na Jaji wa shindano hilo kuwa hadhani kama wanaweza kufika mbali kimuziki lakini leo ni miongoni mwa kikundi kilichojiandikia historia ya kuwa kwenye list ya Forbes kwakuwa na bendi inayolipwa fedha nyingi duniani kwa mwaka 2014.

5: Lady Gaga.


Kwa mara ya kwanza aliposainiwa na label ya L.A. Reid ya Def Jam mwaka mwanamuziki Lady gaga aliwahi kuambiwa na producer wake kuwa muziki wake unakera sana masikioni na hadhani kama muziki ni kipaji chake lakini leo hii Lady gaga ni miongoni mwa wanamuziki waliouza zaidi ya rekodi milioni 10.3.

6: Madona.


Baada ya kuacha chuo akiwa na miaka 17 tu Madona alikwenda jijini New York kujiendeleza kimuziki akiwa na dola 35 tu mfukoni lakini muziki wake ulikataliwa waziwazi na aliyekuwa Raisi wa Millennium Records Jeremy Ienner na kumwambia hamwelewi anachoimba na hadhani kama anaweza kuja kuwa mwanamuziki mzuri.

7: Jordin Spark


Jordin Spark ni mshindi wa shindano la kutafuta vipaji American Idol mwaka 2006 na kuibuka mshindi lakini hakupata ushindi huo na kuwa mwanamziki mkubwa leo hii, aliwahi kukataliwa na majaji wa shindano hilo zaidi ya mara mbili lakini hakukata tamaa alirudia tena na akaibuka mshindi wa shindano hilo kwa sasa.

8: Hillary Scot.


Ni mwanamuziki wa nyimbo za Country ana jumla ya tuzo 7 Grammies ana thamani ya dola million 11 na kuuza jumla ya rekodi milioni 18 duniani kote, kabla ya kuwa mwanamuziki mkubwa Hillary Scot alikataliwa na maproducer wa show ya American Idol na hakupata hata nafasi ya kufika kwa majaji wa shindano hilo.

9: Mary Lambert.


Akiwa na miaka 16 Mary Lambert alishiriki shindano la kutafuta vipaji la American Idol lakini producer wa kipindi hicho Ryan Seacrest alimwambia hadhani kama aina ya uimbaji wake unafaa hata kuingia mzunguko wa kwanza washindano hilo na kumwambia aondoke.

10: Tori Kelly.


Tori Kelly ni mwanamuziki aliyemfanya Jaji wa American Idol Simon Cowel kujutia sana uamuzi wake wa kumtoa Tory kwenye shindano hilo, kwani miezi michache tu baada ya kutolewa kwenye shindani Tory Kelly alitumia mtandao wa Youtube kuonesha kipaji chake.