Thursday 22 January 2015

OYA MWANA, NGUVU HUNA MKWANJA HUNA..HATA MKWARA?

Saluti kwa wanangu wote tunaochekiana kwa mafoni deile kupeana madini ya kuwalisha masela. Inakuwaje kwa kitaa hiyo ya bee machalii? Ni mpango mzima? Selaa huku kwa fasi ya tauni Bongo tambarare watu
tunakabana makoo ileile. Ilimradi tu mwisho wa dei vichwa visomeke. Ama nini? Kaa humu wewe uwe mjanja wangu.
Ebana tudei no mboyoyo mingi kozi laifu liko resi hatare. Kuna mwanangu Chuma au Benz ana bonge la talenti kwenye gemu la miyuziki bati anazingua kinoma! Hataki kukubali kwamba anatakiwa kuchukua makomenti ya vichwa vyake vyenye lavu na yeye dheni kudili nayo ili kusevu laifu. Nimemaliza. Atakuwa amewasoma machalii!
Turudi kwenye mastori moo ya hapa jamvini. Huku na huku nimemingo na kichwa changu Frank niliyemanyana naye kitambo bati tukalostiana. Si unajua tena mbishe za kutafuta laifu? Huyu akiingilia huku mwingine anatokea kule hadi kieleweke.
Miaka ilikuwa imekwenda fasta ileile. Ghafla baba la baba huyu hapa. Mwanangu ananigonga na mkasa wake noma sana aliokutana nao kipindi tumepotezana kwenye sayari hii ya dunia.
Jamaa

ananiteli kwa mahasira kuwa baada ya kulostiana tulipomaliza skuli, alipata mbebi mkareee… Akaona ili amuwini ni beta akamtwanga na kitu cha mereji ili ajihakikishie umiliki. Si unajua zile za kufolu inilavu mzimamzima?
Msela hakuwa mtu wa kuseto mahomu, alikuwa anasafiri mara kibwena kozi mbali na kupiga mbishe za jobu pia ni bizinesmani.Wani dei msela alirejea maisha plasi naiti kali akiwa ametokea kwenye mabizinaa.
Kidume akagonga maskani kwake, akafunguliwa na beki tatu dheni akazama ndani kwa mbwembwe kinoma.
Kaka mkubwa hakuamini alichokiona kwani alimkuta msela f’lani kisharobaro cha kitaa akiwa na mai waifu wake kwenye bedi wakifanya yao.Unajua kilichohapeni mazee? Kaa hapo. Unaambiwa mwana alijiona mnyonge kozi aliishiwa nguvu, hakuwa na mkwanja wa kulipiza na hata mkwara hakuwa nao. Chezea kuibiwa mali zako? Moyo nao una nyama siyo wa chuma so unauma.
Alichokifanya kachaa wangu ni kusepa homu huku akimwachia maza watoto wake kila kitu dheni yupo tauni ameanza laifu upyaaa.Unajua wanangu kuna sampo za makiksi wa kumeri na wengine ni wa kuruka viwanja tu siyo waifu matirio. Sasa mameni wengi wanamaindi kumingo na mashori wakare bila kujua kwamba si wa kumeri. Unakwendakwenda tu bila daireksheni? Itakula kwako mzazi.
Ukicheki kiundani ishu ya mwanangu Frank utanotisi kwamba naye alikimbilia kuoa tu kwa kuwa aliona mtoto mzuri pale kati na rangi adimu. Fulu kuzinguka na mchuchu mkare aibu. Ona sasa anaungaunga na ameshalosti taimu kinoma. Washkaji si mnajua laifu halirudi nyuma? Taimu ikikatika ndo kama hivyo hairudi baki.Ebana eee…wanangu mmenisoma? Ungekuwa wewe ungefanyaje? Tafakari dheni chukua hatua!

Kama vipi sii yuu neksti wiki. Nduki!
KICHEKESHO: MAZUZU YAKIWA BEACH