Thursday 22 January 2015

''NIMEOA LAKINI MKE WANGU ANANIPANGIA RATIBA ZA KUFANYA MAPENZI ''

Mimi ni Kijana wa miaka 30 , Nimeoa mwaka mmoja uliopita , kabla sijaoa nilikuwa najua nikishaoa na kuwa na mke wangu ndani issue ya matamanio ya kimwili itakuwa hainisumbui kwa
kuwa nitakuwa na mke ndani kila nikitaka kitu napata, lakini imekuwa kinyume na nilivyofikiria..kwani nimekuwa mtumwa mke wangu

ananipangia siku gani tufanye mapenzi kwa week mara moja tu , siku zingine hataki kufanya chochote na mimi na nikilazimisha tunagombana na kutishia kuniacha...jamani hii ni sawa ? je nifanyaje ama nitafute demu wa nje?