Wednesday 28 January 2015

OYA MWANA KAMWE MKAA HAUOSHWI!

Niaje…niaje masela wangu? Kitaa hiyo kwa fasi ya kati barida? Mitikasi vipi wana? Kama freshi basi ndo mpango mzima! Ama nini? Basi mzuka kwa wingi chaliiangu.

Karibu jamvini mazee nikusanue ishu bee za kitaa. Machalii hivi laifu mnalionaje kwa saidi yenu? Kipande hii ni fulu mastresi na bado sisomeki aisee arifu.
Tudei bana nitakugonga na limkasa la mwanangu Jeff. Ni kitambo kiduchu kimekrosi. Unajua nini kilihapeni?Mwanangu alizima fegi kwa mtoto mmoko mkare aibu. Yaani mbebiz wa ukwehe kabisa. Si unajua zile za umbo namba nane dheni rangi ya chokleti? Selaa anakuteli kuwa mtoto ni smati kichwani. Sasa ukiwa na shori kama huyo laifu linataka nini tena? Kaa humu wewe upate kitu roho inataka.
asi mtu mzima, kaka mkubwa mwenyewe, akaona ngoja ajaye kwenye kumi na nane za shori. Jamaa akajitoa kitu cha fahamu akaona amepata waifu wa kuspendi naye.Kweli bana, mtoto akajifanya kumwelewa mwana na laifu likasonga fasta kinomanoma. Huku na huku shori akaanza kufosi kitu cha mereji kama ilivyo kwa makiksi wengi wa tauni nawu deizi. Siku hizi ndo zao. Ukijichanganya tu imekula kipande yako na ukitaka kung’oa kirahisi wewe mpromisi mereji.
Diferenti na mbebizi mkare, mwanangu yeye hakuwa na mudi kozi aliona bado taimu ipoipo so hamaindi ishu za kiloko za kuharakisha au kukurupuka. Wazazi asikumiksi mtu maana hutachukua raundi, utaanza kuzinguliwa dheni aibu mazee.
Msela anaamplifai kwamba alipomuwekea ngumu na kumfungukia ukweli kuwa bado yupoyupo sana, mtoto mkare akamaindi kinoma. Jamaa akaona isiwe kitu, akamwaambia anaweza kupita hivi yaani kujivua gamba.
Kweli shori aliuchubua kama wiki bee hivi. Kachaa wangu kitu cha moyo kilimuuma hatari kozi alikuwa amezimika ileile kwa mtoto mzuri.Baada ya wiki bee, uzalendo ukamshinda shori. Akarejesha majeshi dheni akajaribu kumpliizi mwanangu kuwa waendelee na malovee na kwamba alikuwa yupo rede kutumika ipasavyo. Sasa kidume upewe promisi ya aina hiyo na shori mzuri utauliza cha kufanya? Watoto wa mbwa wanakuteli kuwa ushindwe mwenyewe kujilia vyako.
Kweli jamaa aliinjoi mavitu bati leita alishtuka kuwa shori alikuwa na mpango wa kando na jamaa aliyeingia kingi kumpiga kitu cha pingu za maisha.Msela wangu akaona isiwe kitu akamwachia shori akaenda zake kulianzisha na jamaa’ke aliyekuwa akishea naye mambo f’lani. Ebana hakuna soo baya kama kushtukia kuwa shori wako unashea na msela.
Kuliko kushea shori, beta ukauteli moyo uvumilie maumivu bati utemane naye.
Basi bana, shori si akaangushiwa bonge la sendi ofu dheni kitu cha mereji. Kweli watu waligonga mnuso bati tunaposebenza hapa mtoto mkare yupo mahomu kwao ameshamwagwa.
Unajua kilichohapeni?

Mdada anataka kurudi kwa msela wangu kozi ameshamuibukia analia kinoma mazee.
So msela wangu yupo njiapanda amkubalie au amwache atambae? Ungekuwa wewe ungefanyaje wakati inaeleweka kabisa kwamba huwezi kuosha mkaa ili utakate.
Masela tafakarini dheni mchukue hatua. Mmenisoma?
Kama vipi kitu cha wikiendi kwa mbaliii…sii yuu neksti wiki.