Tuesday 16 September 2014

TUHUMA ZA USAGAJI: AUNT LULU AMPIGIA MAGOTI MAMA YAKE SOMA HAPA,


Staa wa filamu Bongo, Lulu Semagongo ‘Aunt Lulu’ amefunguka kuwa skendo ya kujihusisha ya vitendo vya kisagaji inayomuandama imemsababishia msala mkubwa kwa mama yake na kuamua kumuomba radhi.

Akizungumza na paparazi, Aunty Lulu alisema mama yake ana ugonjwa wa presha hivyo amejirekebisha katika eneo hilo ili asiweze kumkwaza tena mzazi wake huyo.
 

“Najua nimemuumiza sana mama yangu, nachukua fursa hii kumuomba sana samahani kwa kuwa najua aliumia sana kutokana na habari hiyo lakini nataka kumuambia kuwa mimi mtoto na nitaendelea kuwa  mwanaye, anisamehe mama yangu,” alisema Aunty Lulu.