Friday 16 June 2017

Man United imeanza na beki wa Benfica (Picha)

Klabu ya Manchester United ya Uingereza imemsajili beki wa Benfica ya nchini Ureno, Victor Lindelof kwa ada ya pauni milioni 31.

Victor Lindelof akiingia mkataba na Manchester United

Huu utakuwa usajili wa kwanza ndani ya kikosi cha Jose Mourinho katika kipindi hiki cha majira ya joto.
Raia huyo wa Sweden amejiunga na United kwa mkataba wa miaka minne akitokea Benfica aliyo jiunga nayo toka mwaka 2012.


Mchezaji mpya wa Manchester United, Victor Lindelof akitambulisha jezi yake



Victor Lindelof akitoka katika vipimo kabla ya kusajiliwa Manchester United 


Victor Lindelof akiwa na mpenzi wake Maja Nilsson baada ya kusaini Manchester United