Monday 28 April 2014

WANAUME WENGINE NI MALIMBUKENI WA KUTONGOZA NA MAPENZI..SOMA HAPA

Leo kuna mwanaume alikuwa nje ya bank mara akamuona binti mzuri anatoka benki.


Akawa amempenda pale alipokuwa nje kulikuwa na gari nzuri toyota 4runner.jamaa akaanza kutongoza uku akiwa kaegamia ile gari na kujisifu ile gari ni yake na akahidi kumpa eti anazo nyingi.

Kumbe hiyo gari ni ya mwanamke mwenyewe anayetongozwa alikuwa ameipaki akaingia benki. Jamaa alikuwa hajui.

Baada ya kumaliza kutongoza na kutoa bznes card.binti akamwambia ebu nipishe akaingia kwenye gari yake na kutokomea. Jamaa akabaki na aibu tele.

Hivi ukimpenda mtu ni hadi ujisifie mali za uongo. Je ukisema ukweli hautopendwa?