Tuesday 15 April 2014

Naombeni Ushauri,Nimfanyeje Huyu Binti

Ilikua jumatatu, tarehe 10 mwezi wa 6 mwaka 2013,niko kwenye msiba wa kaka angu(RIP BRO).. Ilikua kama sa 2 hivi usiku niko kwenye
kikao tukijadili na kupanga taratibu za mazishi,kuhifadhi mpendwa wetu.

Nikiwa kikaoni nikasikia mtetemo kwenye sim yangu ikiashiria ujumbe mfupi umeingia,sikua na haraka ya kuusoma,nikijua baada ya kikao ntausoma,ndio ntakua na muda mzuri wa kusoma ujumbe huo,hata hivyo mimi ndie nilikua katibu wa kikao,nikakipa kikao uzito zaidi.

Ilipofika sa 4 kama na nusu hivi kikao kimeisha, nikasikia mlio wa sim,ilikua ni sim yangu ikiita,nikaitoa mfukoni kuipokea,kusoma jina ni la kipenzi cha moyo wangu,nikatabasam kwa mbali nikijua mpenzi wangu kanipigia kujua naendeleaje,ile napokea tu sim ikakata.

Nikajua mamaa kaishiwa pesa,nikaenda hewani,simu ikaita kidogo kisha nikasikia"simu ya mteja uliepiga inatumika" ikiashiria sim imekatwa,nikakata sim,mara kidogo nikapokea ujumbe kutoka mpenzi wangu

"nilitaka kujua kama meseji umeipata,sitaki mapenzi na wewe,futa namba yangu" nikashtuka kidogo,nikajua ni utani,kisha nikataka kujua ni ujumbe gani huo

Nikaenda inbox nikakuta ujumbe uliokua umetumwa haujasomwa ni wake akinijulisha mimi na yeye basi. Nikampigia sim hapokei,nikatuma ujumbe hakujibu. Msiba wa ndugu yangu ukawa mchungu zaidi

Siku zikaenda hivyo nikiwa siamini kilichotokea,bila ugomvi,bila sababu ya msingi nikawa

nimeachwa. Nikatumia kila mbinu kumbembeleza na kumshawishi,kupitia kwa ndugu zake,marafiki zangu na ndugu zangu akagoma.

Ratiba zetu ilikua mwezi wa kumi mwaka jana nikajitambulishe rasmi,mwezi wa pili mwaka huu tufunge ndoa . Mipango hiyo ikawa imekufa. Niliyumba sana baada ya hilo tukio,nimejikaza nikasimama kiume ila kwa maumivu makali sana.

Kituko cha mwaka ni kua binti huyo kamwambia rafiki yangu kua bado ananipenda na anatamani turudiane, hadi naandika ujumbe huu huyo binti toka juzi anapiga sim(sijapokea simu yake hata moja) na kutuma ujumbe akiniomba nimsamehe

Wadau,nimrudie kisha nimtende kama alivyonifanya au nimuache aendelee na maisha yake(sina hisia nae tena na wala simpendi,,namchukia sana,natamani kisasi juu yake),ebu nishaurini wandugu.