Friday 18 April 2014

USHAURI:KASOMESHWA NA MPENZI WAKE AMBAE NI FUNDI GEREJI,BAADA YA KUPATA KAZI BOSI WAKE NAE KAMPENDA NA KAMUAHIDI VINONO,YUKO NJIA PANDA.

Mimi ninaitwa Aisha, nina miaka 27. Nina mchumba wangu ambaye ni fundi gereji na anaishi maeneo ya Manzese, mi nakaa Tandale. Tumedumu miaka miwili na kusema kweli tulikuwa tunapendana maana hadi kanisomesha kozi ya computer kwa mwaka mmoja sasa nina kazi yangu. Ila nimepata bahati ya mtende maana huyu bosi wangu ninayefanya kazi kwake, ametokea kunipenda sana na amesema nikimkubali, atafanya maisha yangu yawe kama ya malkia. Ahadi za huyu bosi zimefanya nianze kumpenda ghafla maana anatembelea RANGE ROVER kali kama ile ya Lady jay dee, yaani nahisi kuchanganyikiwa sijui nifanye nini? Hapa nilikuwa natafuta sababu ndogo ili nimbwagwe huyu mchumba wangu fundi gereji ila sijapata sababu. Naombeni ushauri wenu kwenye hili