Tuesday 29 April 2014

Mdau anaomba ushauri: Tokea Mume Ameniingilia Kinyume Na Maumbile Sina Raha Naye, Nadai Talaka Lakini Anataka Kuficha Sababu.

Asalamu alekum,Mume wangu alinitaka na kuniingilia kwa nguvu kinyume cha maumbile.Tokea siku hiyo sikua na raha kwani alinilazimisha na wala
sikutaka,alinikamata kwa nguvu.Sina mapenzi nae tena na nimemwambia anipe talaka yangu.Hataki kuniwacha na imekua ugomvi ambao umefika mpaka kwa wazee lakini ameniomba na kunishikilia nisiliseme jambo hili kwa wazee wa pande zote mbili kwa kuchelea kujiharibia heshima yake. Nimelikubali hilo lakini simuoni kama mume kwangu mapenzi hayapo tena kwangu. Nifanyeje?