Thursday 15 June 2017

Adele awafariji wahanga wa moto Uingereza

Msanii Adele wa Uingereza ametembelea katika ghorofa la Grenfell Tower lililoteketea kwa moto Jumatano hii kwa kuwafariji wahanga.

Picha ya Adele akiwa ametembelea eneo la Grenfell Tower

hitmaker huyo wa ‘Hello’ amekuwa msanii wa kwanza kutembelea katika eneo hilo la ghorofa 24 lililoteketea kwa moto na kusababisha vifo vya watu 12 na wengine 18 wapo mahututi wamelazwa katika hospitali saba tofauti ikiwemo St Mary’s, Chelsea, Westminster, Royal Free, St Thomas’, Charing Cross Hospital na King’s College Hospital.


Adele ameahidi kuwasaidia wahanga wa tukio hilo. Hata hivyo mtangazaji na muigizaji wa nchi hiyo, Jamie Oliver ameungana na Adele kutangaza kuwasaidia wahanga hao.