Thursday 15 May 2014

UTAFITI UNAONYESHA HIZI NDIZO SABABU ZA WANAWAKE WENGI KUPENDA KUVAA NGUO ZA NUSU UTUPU..SOMA HAPA KUZIJUA

 

Wakati mwingne wanaume au watu tofauti hudhani kwamba, wanawake wanaovaa nusu uchi huwa wanafanya hivyo kwa sababu ya kutafuta soko kwa wanaume.

Inawezekana kukawa na wale ambao wana sababu hizo, lakini wapo wale ambao wanalipa fidia kutokana na kuamini kwao kwamba wanamapungufu kwa mfano sura zao zimewaangusha, hivyo miguu yao mizuri inabidi kuziba pengo au udhaifu huo. 

Wakati mwingine hata wanawake wanaodhani au kudhaniwa kuwa ni wazuri, wamekuwa wakivaa nguo fupi zinazoonyesha maungo yao.Hawa nao ni lazima wanalipa fidia ya kasoro fulani waliyo nayo.

Inawezekana wameshindwa kulinda ndoa zao, au inawezekana hawajaolewa na sasa wanataka kuonyesha kwamba, pamoja na kutoolewa kwao, bado wao wana sura na miguu au miili mizuri.

Wangapi Mnakubalia na Mimi ?