Thursday 22 May 2014

MWANAUME FANYA HAYA KAMA UNATAKA KUEPUKA KUCHUNWA NA WANAWAKE

Naongea na wale ambao tayari wamesha jitegemea kimaisha, ambao hawaishi na 
wazazi wao, wanaokumbana na mkono wa Mama/Baba mwenye nyumba kila
baada ya miezi sita mitatu au mwaka..

Wanaoishi ki-bachelor lakini wana wapenzi.

Katika hii movie ya ki-bachelor wanakumbana na mengi sana,,kuna wanaogeuza ma girl friend zao kuwafanya kama mke,,tabia ya aina hii imepelekea na wao kugeuzwa kama waume,,hapa unakuta kila kitu girlfriend anakutegemea wewe akipata kashida kidogo ooohh baby nataka hela..


Mazingira ya kuchunwa tunayatengeneza wenyewe usianze kumhisi binti wawatu ni mchwa,,jichunguze kwanza na wewe kinachofanya akunyoshee mkono.
Ukiweza kuyamudu mambo haya hakika hautayachukia maisha ya ki-bachelor na kumgeuza girl friend kuwa mke, na yeye pia atashindwa kupata ujasiri wa kukutegemea kiasi fulani labda tu kama nitabia yake..
1. Kujipikia
2. Kufua
3. Usafi wa vyombo.
4. Usafi wa chumba.
Ukiweza kukabiliana na hayo pasipo kutegemea msaada kutoka kwa girl wako utayafurahia sana maisha ya ki-bachelor,,na swala la kuoa kwako utaliamua kwa wakati muafaka, ila sio kwa kuwa unahitaji msaidizi.


Ebu fikiria labda girlfriend wako anakuja kukusalimia siku ya mapumziko, anakuta chumba chako umesafisha vizuri vyombo viko katika mpangilio mzuri,,umefua nguo zako na mashuka,,huku na huku haujachoka kuna akiba ya mchele,,unawasha kajiko kako unapikia wali na unaandaa mboga yani kila kitu unaweka sawa kisha unapakua kwenye hotpot yako, basi akija mnakula kama atapenda,,baada ya chakula mnaendelea na mambo yenu,,kusanya vyombo vyako akiondoka unaviosha.


Kumbuka kufanya hivyo hakuondoi uanaume wako,jifunze kudhamini vitu vyako girlfriend hajawahi kukununua hata kijiko vyote umenunua kwa pesa yako,,ulio itolea jasho kwa kugombania daladala asubuhi uwahi kazini.

Hapo unajaribu kutengeneza mazingira ya kumfanya asijihisi unamtegemea sana zaidi ya kitu kimoja tu nadhani unakijua kwa wale mabachelor ambao mnamiliki kiwanja cha fundi selemara chumbani kwako.


Kama bachelor mwenye akili zako timamu lazima uishi kwa malengo ukijua kesho na wewe utakuwa na familia itaishi vipi kama ukiendekeza kuhonga katika ubachelor wako.
 

Ishi na mwanamke kwa kanuni kama unavyo fanya hesabu,,baada ya hayo kinachofuatia hakikisha unatumia kiasi kidogo sana cha pesa kumnunulia vitu vidogo vidogo ambavyo havina gharama,,ili mkusahaulisha kiasi fulani auone uwepo wako.
 

Ila kama wewe sio muoga kama mimi basi unamkazia kabisa,,maana demu nae akishajua unapenda pochi manyoya yake basi atakubabaishia,,,usiwe mtumwa wa pochi manyoya.


Kwa style hiyo binti unasababu ya kumtegemea boy wako???

Na wewe bachelor mwenzangu hapo bado unayo sababu ya kugeuzwa kitega uchumi