Wednesday 21 May 2014

JAMANI MABOSI WA KIKE PUNGUZENI KUKAA UCHI UCHIIII LOO!

Imezuka tabia ya ajabu sana kwa baadhi ya mabosi wa kike ambao wanatokea kuwazimia vijana wabichi aka Serengeti boy matokeo yake mabosi hawa huanza kuwatega kwa namna mbalimbali.
Katika Ofisi moja iliyopo maeneo ya Posta nilipata bahati ya kufanya mahojiano na mkaka mmoja Mtanzania jina lake ni Kwilasa ambaye amemaliza shahada yake ya computer science katika chuo kikuu cha Missisipi nchini Marekani miaka mitatu iliyopita.
Ni handsome kwelikweli lakini anatokea kukosa raha na amani na kazini kwake kwani katika ofisi nyingi alizowahi kufanyia kazi huwa anakasumba ya kutakwa na mabosi wake wa kike ambao maranyingi huwa wameolewa na wakati mwingine wanafamilia zao.
Kaka huyo kila anvyojitahidi kuepusha shari kwa kutojenga mazoea nao lakini haisaidii kwani mabosi hao wamekuwa wakitumia njia tofauti za kumfanya awe karibu kwa kutumia amri kama bosi na hivyo kaka huyo kushindwa kupinga chochote kwani ni sehemu ya kazi yake.
Juzi juzi kaka huyu amepatwa na majaribu zaidi pale alipopigiwa simu na sekretari wa bosi kwamba anahitajika ofisini kuna kompyuta imepata hitilafu ya programu hivyo haraka anahitajika ofisini kwa bosi wake.
Kijana huyo bila kusita aliwahi haraka ofisini hapo lakini pozi alilomkuta bosi wake sio zuri hatakidogo kwa mwanaume yoyote rijali kwani bosi alikuwa amepanua miguu pale kwenye kiti,mapaja yake meupe na yakuvutia yalikuwa yameanikwa njenje yaani  kama wadada wanaocheza video za ngono.
Kwilasa alijitahidi kufanya kilichompeleka lakini bosi wake huyo aliibua shida mbalimbali za kompyuta yake ambazo sio wala za msingi ilimradi tu kaka huyo azidi tu kuwepo humo ofisini.
Kaka huyu  alishapeleka malalamiko kwa HR Manager lakini haikusaidia kitu kwani bosi ni bosi na ukimletea mchezo waweza kukosa kazi jambo ambalo linazidi kumweka njia panda.  Unaushauri gani kwa huyu kaka ili afanye maamuzi sahihi?