Monday 26 May 2014

Sumu ya Mwanamke ni Mwanamke Mwenzie.....!!!

Usemi huo nilikutana nao kijiweni, wazee wakipongeza uamzi wa dini kuwa na wake wanne, kwamba mwanamke akijua kuna mwanamke mwenzake basi ananyoka vizuuuuriiii,
hutasikia habari za usawa katika familia.
Maneno haya nimeyaamini baada ya kisa hiki kunitokea, nipo na mpz wangu nampenda sana
na nimejiapiza ndo atakuwa mke wangu, kuna wakati akaanza kunisumbua, nilichokifanya ni kujenga mazingira nataka kurudiana na x wangu, kwamba ananibembeleza sana na hata anatumia ndugu zangu kunishawishi turudiane, kwa kweli nampiga fix tu, tokea nioneshe hivyo mpenzi wangu kanyooka kama mti wa muashoki, ule usumbufu wake wa mwanzo umekwisha kabisa, ananibembeleza kama mfalme. 

Nimeamini SUMU YA MWANAMKE NI MWANAMKE MWENZIE.