Monday 26 May 2014

USALITI KATIKA MAPENZI UNAUMIZA SANA,,UNAJUA KWANINI! INAKUWA HVI......

Usaliti katika mapenzi unaumiza sana..kwa 
nini inakuwa hivi? 
Wanaume wengi wanapobaini kuwa 
wapenzi wao wanawasaliti, hutunisha 
misuli kuonesha umwamba kwa 
kuwatwanga makonde wapenzi wao au 
kuwafanyia mbaya wale waliowanasa. 
Lakini uchunguzi wa wana mapenzi 
unaonesha kuwa ubabe haukomeshi tabia 
ya usaliti. 
Kuna wengi ambao waliwafumania wake 
zao, wakawapiga na kuwajeruhi, lakini 
wakajikuta hawakukomesha tatizo, zaidi ya 
kuwapa usugu wapenzi wao wa 
kuendeleza wizi tena kwa dharau na kejeli 
huku wakibembelezana kwa maneno haya: 
"mzushi kaenda kazini njoo sasa hivi 
Wapendanao Gesti" au "vipi yule bwege 
alikuuliza jana ulipochelewa kurudi" Jamaa 
anaweza kumuuliza hivyo mke au mpenzi 
wa mtu. 
Katika hali ya kawaida usaliti ni jambo 
linalouma kwa kiwango kikubwa. Katika 
mapenzi hakuna suala la kuazimana mume/ 
mke. Watu huazimana magari na pesa, 
lakini laazizi hakuna jasiri wa namna hiyo! 
Hivyo ndivyo lakini, kupiga au kuachana 
baada ya kufumaniana kunasaidia? Jibu 
hakusaidii, kwani ukimpiga adhabu inaishia 
hapo hapo, kesho yake watakaokutana 
watakusaliti tena kupozana machungu. 
Maamuzi ya kuacha naye hayasaidii kwani 
ukimwacha mpenzi wako hujamtibu, 
utakuwa umetoa mwanya wa yeye 
kuendelea kukusaliti na kukuumiza zaidi 
pale macho yako yatakapowaona 
wameshikana mikono mitaani kwa uhuru 
na raha zao. 
Ukiamua kuua na wewe utauawa, huku 
wanadamu wenzako wakikucheka kwa 
uzembe wa kufikiri. Jamani usaliti upo kila 
siku, si tunawaona wake na wapenzi wa 
watu wanaingizana gesti kila siku? 
Hivyo, kama hujamfuma mpenzi wako leo 
kuna siku utakutana na meseji kali 
akibembelezana na 'kidume' mwingine kwa 
maeneo fulani. Utafanyaje baada ya kubaini 
hivyo, maana kama ni tukio basi utakuwa 
umeona lile la stejini laivuuuuuu bila 
chenga. Twende pamoja ili tuelimishane 
kama wadau wa mapenzi njia sahihi ya 

kufanya ili kumwadhibu mpenzi msaliti. 
Kwanza, baada ya kuwaona uso kwa 
macho wakisaliti penzi, unatakiwa kutoa 
ishara zitakazoonesha kuwa umewaona, 
halafu ondoka eneo hilo. Ukifika home mtu 
mzima endelea kunywa maji ili kupoza 
presha. Akirudi mpenzi wako jitahidi 
kumkaribisha kwa bashasha, lakini 
usimuulize ulichoona mwache aendelee 
kujiuliza mwenyewe. 
Au kama umenasa meseji za kimahaba 
kutoka 
kwa mwizi wako, zitume kwenye simu yako 
kwanza, kisha baada ya kumaliza 
uchunguzi wako mtumie tena sms hizo 
mkeo/mumeo. Ukifanya hivyo usimuulize, 
endelea kumpenda na ikiwezekana ongeza 
matunzo. Nunua 'mikuku' akaange kila siku 
na umpe penzi moto moto. 
Nakwambia ukifanya hivyo mpenzi wako 
ataumia sana na hataendelea kukusaliti 
kwa kuwa atakuwa anawaza unafikiria 
kumfanya nini? Na kwa yule uliyemshika 
naye, vivyo hivyo usizozane naye, mwache! 
Utashangaa anahama eneo maana atakuwa 
anafikiri unamwandalia kombora kumbe 
wewe wala, umeamua kujituliza tu! 
Wadau wa mapenzi hii ndiyo dawa ya mtu 
msaliti. Mwadhibu kwa upole, 
wanasaikolojia wameithibitisha adhabu hii 

kuwa ina uchungu mara 1,000 zaidi ya 
kupiga au kukemea. Ukisema umwache 
siyo dawa kwani unaweza kutafuta 
mwanamke/mwanaume mwingine naye 
akawa na tabia zile zile, ikiwa ndivyo 
utaacha wangapi basi katika maisha haya? 
Adhabu ya mpenzi anayekusaliti ni 
kumnasa kwenye usaliti wake kisha 
kumpuuza huku wewe ukiendelea na 
mambo yako kama kawaida, ukifanya hivyo 
utakuwa unamtibu ugonjwa wake wa 
kupenda penda hovyo na hii ndiyo dawa 
hasa ya kumponya msaliti, lakini pia 
inasaidia kupunguza maumivu ya penzi. 
Kumchunga na kumlilia machozi hakusaidii.