Wednesday 20 August 2014

TIKO: WAUME ZA WATU SASA BASI!

MSANII wa filamu Bongo, Tiko Hassan amesema ameamua kuachana na tabia ya kuwa kimapenzi na waume za watu kwani ameona wanachosha na uhusiano huo hauna uhuru tofauti na ule wa aliye singo.

Msanii wa filamu Bongo, Tiko Hassan.
Akipiga stori na paparazi wetu, Tiko alisema ameamua kuachana na uhusiano wa
kimapenzi na waume za watu kwani alikuwa na mume wa mtu lakini hakuona faida yoyote zaidi ya kukosa uhuru kutokana na kuhofia kubambwa na mwenye mali.
“Nimeamua kuachana kabisa na waume za watu kwani hakuna raha yoyote, yaani nilikuwa nakosa uhuru kabisa wa kujiachia na mpenzi wangu huyo hivyo kwa sasa nimestaafu, sitaki tena kuwa na mume wa mtu,” alisema Tiko.