Thursday 21 August 2014

MMH DJ FETTY BALAA AZICHAPA LIVE NA MREMBO HUYU


MTANGAZAJI wa Clouds Redio na TV , Fatuma
Hassan ‘ DJ Fetty ’ , juzikati alijikuta
akitwangana makonde na mrembo mmoja
ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara
moja baada ya kupishana kauli kwenye
ukumbi mmoja wa starehe pande za Kahama,

Shinyanga. Katika tukio hilo, Fetty aliyekuwa kwenye ‘ tour’
ya Serengeti Fiesta alizama ukumbini hapo
usiku na baada ya muda mfupi paparazi wetu
alishangaa kumuona akizichapa na mrembo
huyo ikidaiwa walizinguana
, hata hivyo
waliamuliwa kabla mambo hayajawa mabayaw .
Ziara ya Tamasha la Fiesta kesho itahamia
Tanga ambapo wasanii kibao wataangusha
burudani ndani ya Uwanja wa Mkwakwani .