Friday 22 August 2014

MWANAMITINDO AISHTAKI KAMPUNI KWA KUONYESHA SEHEMU ZAKE ZA SIRI HADHARANI

Mwanamitindo Jessie Nizewitz ambaye alikuwa kati
ya wasichana waliokuwa kwenye mashindano ya
series ya ‘Dating Naked’ amefungua mashitaka
dhidi ya makampuni yanayowezesha show hiyo
kwa kurusha vipande vinavyomuonesha akiwa
mtupu bila kuficha sehemu zake za siri.

Katika shitaka hilo, Jessie anadai fidia ya $10
million kutoka kwa makampuni ya Viacom, Firelight
Entertainment, Lighthearted Entertainment kwa
kushindwa kuficha kwa kuweka blur kwenye
maeneo ya sehemu zake za siri kama
walivyokubaliana awali.
“Ingawa niliingia kwenye shindano hilo nikijua
kuwa ningeshuti nikiwa mtupu, niliambiwa
kuwa
sehemu zangu za siri zingefichwa kwa kuwekewa
blur kwa ajili ya show ya TV…hata washiriki
wengine hawakutegemea kuona hivyo.” Alisema
Nizewitz.
Kipande cha show hiyo kinachomuonesha
mwanamitindo huyo kilirushwa July 31 mwaka
huu.