Wednesday 28 September 2016

Wanaume wa siku hizi mbona mnalia lia sana kuchunwa?

Hata maandiko matakatifu yameandikwa mwanaume utahangaika juani ili umlishe mkeo na mwanamke atazaa kwa uchungu, sasa imekua siku hizi wanaume kumhudumia mwanamke imekua ni kulia lia sana mwanaume wa ukweli anatakiwa ajue mpenzi wake au mke anamhudumia vipi.

Hivi mnadhani nyie wavulana unakua hujaoa una mpenzi tu unataka aishi vipi unakuta unatoa vielfu 50 unalalamkika mpaka povu linakutoka unataka kumiliki msichana mrembo mzuri huku unatoa kihamsini unalalamika sana starehe gharama ukiona vyapendeza ujue vimegharamiwa.

Ebu kueni wastaarabu basi kutwa kulia lia humu JF, mnawadhalilisha sana kina dada anakuja kwako kajigharamia mwenyewe mapouda nini unamgaragaza unamtindua wewe ukimpa kihamsini unalalamikaaaaaa sasa unatakaje?

Acheni hizo basi ukimtoa out akija na rafiki yake wakinywa savana tu mnalia sasa mnataka wanywe viroba? Au safari?