Thursday 29 September 2016

SASA UKIONESHA MAKALIO HADHARANI UTAAMBULIA KWENDA JELA

Kuonyesha makalio hadharani sasa ni uhalifu katika jimbo la Victoria nchini Australia.
Hatia hiyo inayojulikana kama ''mooning'' kwa lugha ya kiingereza sasa ina hukumu ya hadi miezi sita jela .

Marekebisho ya sheria hiyo yanalenga kutenganisha utani unaohusisha uchi na ule wa kujionyesha kingono.

Sheria hiyo mpya pia inapiga marufuku uimbaji wa nyimbo chafu pamoja na tabia nyengine zinaozoonekana kuwa za uasherati, uchafu, kukera au kutusi.