Thursday 8 September 2016

Vitu Ambavyo Mwanamke Anataka Kutoka Kwa Mwanamume Yeyote

Wanaume wengi hubaki kujiuliza ni vitu gani ambavyo wanawake hupenda -lakini kila wakati wanapokea majibu tofauti tofauti yasiyokuwa na mwisho. Kadiri wakati unapobadilika, wanawake pia hubadilika. Na kuongezea ni kuwa kila mwanamke analadha yake tofauti na mwingine...so kiufupi wanawake huwa tofauti na wengine na hauwezi kusema wanawake wote huwa wanatafuta kitu kimoja kutoka kwa mwanamume. Lakini kama kawa, hatuwezi kukosa vitu ambavyo vinapatikana katika wanawake wote. Wanawake kwa kawaida wana tabia flani ambayo hupatikana kwa kila mmoja wao. Najua mpenzi wako labda unataka kumpenda ukiwa naturally...yaani vile ulivyo kitabia. Lakini kuna mambo mengine ambayo mwanamke angependa uwe nayo ambayo kwa sasa huna so ni lazima ukazani ili uwe na baadhi ya tabia hizo. Na kama uko nazo basi wewe ni miongoni mwa wanaume ambao wanapigiwa upato na wanawake wengi. Cheki list yenyewe ya tabia ambazo mwanamke yeyote angependa kumwona mwanamume akiwa nazo.

1. Kuwa gentleman ama mwanamume thabiti
Wanawake siku hizi wamekuwa wa kisasa, lakini bado wangependa kuwa na mwanamume ambaye anawafungulia milango, wanawaletea saprize mara kwa mara nakadhalika. Pia wanapenda mwanamume ambaye ni mkarimu na ambaye ni mpole. So kama wewe unatabia za ugentleman, basi una nafasi kubwa ya kumridhisha mwanamke yeyote. Na kama huna hizo tabia basi kazi ni kwako. 

2. Kuwa mtu mwenye hisia na mambo ya kwake
Kama tulivyotangulia kueleza hapo juu ni kuwa mwanamke anapenda mtu mwenye tabia za kigentleman, so kama wataka kuyeyusha moyo wa mwanamke ni kuhakikisha kuwa unapenda kumfanyia saprize mara kwa mara huku ukimuonyesha ukarimu wako kwake. Hii itasaidia kumfurahisha na kutimiza ndoto zake. Kumfanya kuwa special ni dhahiri kuwa utamfanya akupende zaidi na zaidi.

3. Kuwa na tabia za utu uzima
Kulingana na utafiti ni kuwa wanawake wengi hupenda kudate na wanaume ambao ni wakubwa kuwaliko. So kama wewe unajiona unatabia za utuuzima na hauna mambo ya kifala basi bila shaka utatimiza ndoto yako na kuwa na yule umpendaye.

4. Kujiamini
Mwanamume ambaye anajiamini kuwa yeye ni yeye bila kujishuku ana nafasi kubwa ya kuteka hisia za mwanamke yeyote. Kujiamini hakumaanishi kutojali na mambo yeyote bali kujiamini kinafsia. Mwanamume anayejiamini anaweza kukabiliana na matatizo yeyote ambayo yanaweza kumkumba maishani mwake. So hio ni rahisi kwa mmoja kuiteka hisia a mwanamke kiurahisi. 

5. Kuwa na uwezo wa kumshughulikia
Wanawake wanafikiria maisha ya mbele, yaani maisha ya usoni mkiwa nyote wawili. So mwanamume ambaye anaonyesha dalili za kuwa anajielewa na ana uwezo wa kumtunza yeye kifedha maishani basi ana nafasi kubwa ya kumnasua mwanamke kiurahisi. Ujue kwamba hii haimaanishi kuwa lazima uwe tajiri kuweza kutimiza ndoto yako bali kile unachohitajika ni kumsaida kadri unavyoweza wewe na usipitishe kiwango ambacho kinaweza kukuathiri kisaikolojia.

6.Uwe nadhifu 
Ingawa kuwa nadhifu haichangii sana kumfurahisha mwanamke kama ilivyo kwa wanaume, bado hii ni baadhi ya vitu ambavyo mwanamke angependa kuviona kwa mwanamume yeyote. So kufanya akupende lazima uhakikishe umetia bidii fulani katika sekta hio. 

Sasa, hata kama kuna tabia flani hapa tulizozieleza ambazo hazifanani na wewe kabisa, haina haja ya kujistikia vibaya. Ili mradi una nia ya kujifundisha kuwa na tabia kama hizi ama unauhakika kuwa mbeleni utakuwa na tabia kama hizi, basi wewe una nafasi kubwa zaidi ya kukufanya kupendwa na wanawake ambao wako wengi wanatafuta wanaume ambao wanatabia kama hizi.