Tuesday 13 September 2016

DALILI ZA UKOSEFU WA NGUVU ZA KIUME, NA JINSI YA KUKABILIANA NALO


Habari msomaji wa www.dkmandai.com kama utakuwa ni mfuatiliaji mzuri basi utakuwa unafahamu kuwa tayari tulianza kuzungumzia tatizo hili la upungufu wa nguvu za kiume na tulizungumzia sana kuhusu sababu za tatizo, leo tuangazie dalili zake pia. Karibu 

Dalili za tatizo hili si rahisi kuonekana endapo mtu atakuwa hashiriki tendo hilo. Hii ni kwasababu suala la nguvu za kiume ni ukamilifu wa tendo, lakini wengi hufanikiwa kushiriki tendo shida inakuja kwenye kulikamilisha tendo au kushindwa kusimamisha.

Mbaya zaidi wanaume wengi wamekuwa wakijitathimini ubora wao katika tendo kulingana na saa wanazoweza kufanya tendo hilo, lakini hiyo si njia sahihi ya kipimo cha uwezo wa kushiriki tendo hilo.

Kimsingi muda si kipimo cha nguvu za kiume, nguvu ni ule uwezo wa kukamilisha lile tendo kuanzia mwanzo hadi mwisho, unaweza ukawa umechukua sekunde mbili, lakini kama umelifanya na likakupa matokeo yale yanayostahili basi hilo tendo ni kamilifu halina mapungufu yoyote

Pamoja na hayo, suala hili pia hutegemea sana namna ulivyojiandaa kisaikolojia katika siku ya tendo hilo. 

Kwa mfano siku umechoka sana na unapokosa hamu ya tendo la ndoa basi tegemea kuchukua muda mrefu zaidi kumaliza, lakini siku ambayo utakuwa umejiandaa kisaikolojia itakuchukua muda mfupi kumaliza tendo, kwa sababu kuna uhusiano mkubwa kati ya tendo na fikra za mtu.

Udhaifu wa tatizo hili huweza kubainika endapo mhusika atakuwa akishindwa kufanya tendo hilo kwa kila mwanamke na endapo hali hiyo itakuwa ikijirudia mara kwa mara.
Hata hivyo, ni vizuri jamii hususan vijana wakafahamu tatizo hili huchangiwa na maandalizi hafifu ya tendo hilo. Hivyo kitu muhimu ni maandalizi ya kutosha. 

Pamoja na hayo, imefika wakati sasa wa kujenga tabia ya kupanga ratiba ya matendo ya ndoa na siyo kukurupuka tu, lakini pia kuna umuhimu mkubwa wa kutibu magonjwa yote bila kujali ni ya ngono au la! Jambo ambalo husaida kupunguza tatizo hilo. 

Pia tatizo hilo huweza kudhibitiwa kwa kula vyakula asilia hususan vya nyuzinyuzi ambavyo vimesheheni nishati nyingi. 

Vyakula vya nafaka husaidia kuzalisha homoni za ‘testosterone’ kwenye damu pamoja na kumuwezesha mhusika kuwa na nguvu na hatimaye kuongeza kiwango cha uwezo wa kushiriki tendo. 

Ulaji wa nafaka zisizokobolewa hufaa zaidi kiafya kuliko zile zinazokobolewa kwani husaidia kuupa mwili nguvu zaidi na hivyo kusaidia kuongeza uwezo wa nguvu za kiume. 

Tangawizi nayo ni kiungo kizuri na muhimu katika kuongeza nguvu za kiume, kwani husaidia kusisimua mfumo wa mzunguko wa damu mwilini. 

Damu inapozunguka vizuri mwilini huwezesha kufika kirahisi sehemu za viungo vya uzazi ikiwa ni pamoja na uume. 

Matumizi ya mbegu za tikiti maji zilizochanganywa na mbegu za maboga nazo husaidia sana kuimarisha na kuongeza nguvu za kushiriki tendo la ndoa. 

Pia tunda la komamanga nalo ni zuri katika kuimarisha masuala haya ya tendo la ndoa hususan upungufu wa nguvu za kiume. 

Ulaji wa tunda hili huamsha mishipa ya damu na hivyo kuimarisha mawasiliano mazuri ndani ya mwili na kusaidia kuongeza hamasa ya tendo. 

Vyakula vingine ambavyo ni muhimu katika kuimarisha tendo la ndoa na kuongeza nguvu za kiume ni pamoja na karanga, ambazo zina kiwango cha madini ‘magnesium’ na zinki ambayo yana umuhimu mkubwa katika uzalishaji wa mbegu za kiume. 

Mbali na vyakula hivyo, asali nayo hufaa kwa mtu mwenye shida ya upungufu wa nguvu za kiumea ambaye anaweza kuamua kila siku asubuhi na jioni akawa anapata angalau kijiko kimoja cha chakula cha asali