Tuesday 6 September 2016

AIBU JAMANI! MUME ANASA PICHA CHAFU ZA MKEWE NA MSANII WA BONGO MOVIE

MAMA Fanueliii! Mwanamke Elgiva Winyaeli Munisi ‘Manka’, mkazi wa Kijitonyama, Dar, amejikuta katika wakati mgumu baada ya mumewe, Alpha kudaiwa kuzinasa picha za utupu akiwa na mchepuko uliofahamika kwa jina la Crama Lucas ambaye ni msanii wa Bongo Muvi, Ijumaa Wikienda lina filamu kamili.
Elgiva Winyaeli Munisi ‘Manka’ na mchepuko wake Crama Lucas ambaye ni msanii wa Bongo Muvi, wakipozi kimahaba.Chanzo makini kimeliambia gazeti hili kwamba, awali, mwanaume huyo alizibamba picha chafu za mwanaume peke yake zikiwa kwenye laptop ya mkewe ambapo alipomuuliza alijitetea si zake ni za rafiki yake alimtumia yeye kupitia Mtandao wa WhatsApp.
MUME AJIONGEZA
Iliendelea kudaiwa kuwa, mume alimuuliza rafiki aliyetajwa ambapo awali alikataa kumtumia picha hizo Manka, lakini baadaye alikiri jambo ambalo mume alijiongeza akiamini lilipangwa.
MACHALE YAMCHEZA
Ilidaiwa kuwa, mume alimkalisha mkewe na kumwambia alichofanya ni kosa kubwa katika ndoa, mambo yakaisha.
Chanzo kilitiririka: “Lakini mume akawa bado machale kama yanamcheza kwani aliingiwa na wasiwasi mkubwa kuamini kuwa, mkewe anaweza kuhifadhi picha chafu za mwanaume kwenye laptop.
“Siku moja, mumewe alikwenda kwenye stationery (duka la vifaa vya kuandikia) inayomilikiwa ya dada yake Manka (jina tunalo) maeneo ya Sinza-Mori (Dar).
“Alipofika aliwauliza wafanyakazi kwamba mkewe akienda pale hukaa kwenye kompyuta gani! Wakamwonesha, akakaa, akasachi jina la mkewe likatokea folda lenye picha kibao za mkewe huyo akiwa na Crama tena kwenye mapozi ya kimahaba. 
MUME APAGAWA
“Palepale mume alipagawa, kidogo presha imshike. Alimpigia simu mkewe akamuita aje pale alipo lakini mke alisema ana kazi nyingi nyumbani hawezi kutoka. Mume alitoka hadi nyumbani kwake na kumuuliza mke wake kuhusu picha hizo, mke akadai mwanaume huyo ni mteja wake wa mashuka! Mh!
“Hasira zilimpanda mwanaume, mteja gani wa mashuka hadi kupiga picha? Alimpiga mkewe hadi kumpasua sehemu ya paji la uso na kumchomea nguo moto. Mke akakimbilia Kituo cha Polisi Kijitonyama ‘Mabatini’, Dar kushitaki lakini baadaye alifuta kesi.” 
MUME ASAKWA
Baada ya madai hayo, Ijumaa Wikienda lilimsaka Alpha, alipopatikana alikiri kuwepo kwa mgogoro kati yake na mkewe chanzo kikiwa ni hizo picha chafu alizopiga mkewe na zile alizopiga akiwa na mwanaume anayedaiwa kuwa ndiye mchepuko wake.
“Awali, nilizifuma picha za utupu za mwanaume nikaamua kumpeleka mke wangu kwao akapumzike lakini wazazi wake walimuonya, akarudi tukawa tunaendelea na maisha, sasa sijui amekumbwa na nini mpaka leo hii akatoka nje ya ndoa wakati mimi nipo na ukizingatia ni mtu ambaye nimetoka naye mbali.
“Mpaka nazikuta hizi picha sikuamini kabisa kama mke wangu anaweza kunifanyia hivi. Sijui walipigaje kwanza, lakini niliumia sana nikaamua kumpiga mpaka akachananika usoni na nilimchomea nguo zake zote kwa sababu nilikuwa nina hasira.”
MUME BADO
“Tangu siku hiyo mke wangu aliondoka nyumbani, mpaka sasa hivi anaishi kwa dada yake lakini kila nikimuomba arudi nyumbani anakataa na kudai kuwa anaogopa nitampiga, ila nilishaongea na yule mwanaume na nikamtaka tuonane akaniambia hawezi kuonana na mimi.
“Pamoja na yote, bado ninampenda mke wangu kwani sitarajii kufunga ndoa na mwanamke mwingine,” alisema Alpha.
Kuhusu uhai wa nyumba yao, Alpha alisema alifunga ndoa na Manka mwaka 2009 katika Kanisa la Anglikana Chimuli, Dodoma.
CRAMA ASAKWA 
Kwa upande wake, Crama alipotafufwa kwa simu na gazeti hili kuhusu madai hayo, alisema:
“Mimi na Manka tunafahamiana kwa muda mrefu tena ni rafiki yangu kwa sababu tulifahamiana kupitia Mtandao wa Kijamii wa Instagram na alikuwa akinikopesha mashuka.
“Alikuwa anakuja sana nyumbani kwangu kudai madeni yake lakini yeye mwenyewe ndiyo alikuwa akinishinikiza tupige picha tena kwa kutumia simu yake.
“Sikujua kama ni mke wa mtu wala yeye mwenyewe hakuwahi kuniambia kama ameolewa na wala hakuwa na pete ya ndoa, ila nilishawahi kumwambia kuwa picha tunazopiga zisije zikazua balaa baadaye, hakuonesha mshtuko.
“Niliwahi kupigiwa simu na mume wake akidai kuwa nilikuwa nikimuibia mke wake, kumbe si kweli kwa sababu Manka mwenyewe anamfahamu mchumba wangu.”
HUYU HAPA MANKA
Manka alipotafutwa juzi kujibu tuhuma hizo kupitia simu yake ya mkononi alidai kuwa hawezi kuzungumzia suala hilo kwa muda huo mpaka atakapojipanga:
“Siwezi kuliongelea hilo sasa hivi mpaka pale nitakapojipanga na kujua hizo picha zimefikaje hapo ofisini kwenu.”