Tuesday 20 September 2016

DHAMBI YA KUMLIZA, KUMTESA ANAYEKUPENDA KWA DHATI!

Mpenzi msomaji wangu, hakuna ubishi mapenzi yanachukua nafasi kubwa katika maisha yetu. Mimi na wewe tunahitaji kuwa na wapenzi tena wenye mapenzi ya dhati ili maisha yetu yaweze kukamilika. Bila kuwa na mtu ambaye kuna wakati unammis, ukiwa naye unajiona ni mwenye bahati kwa faraja anayokupa, ni lazima utahisi umepungukiwa kitu muhimu.Lakini wakati ukweli ukiwa hivyo, wapo wanaochukulia mapenzi kama kitu rahisirahisi. Kitu ambacho anaweza kuingiza usanii na mambo yakaenda. Hapa namaanisha hivi, mtaani kuna watu wa aina mbili. Kuna ambao wanajua kweli kupenda. Akisema anampenda fulani, anamaanisha na kuna wale ambao…