Sunday 11 September 2016

Kumfanya Mwanamke Aanze Kukukiss Wa Kwanza

Kuna mmoja wa readers wetu wa dhati wa Nesi Mapenzi alishindwa kujizuia na aliamua kututumia ujumbe kuwa anaswali ambalo linahitajika kujibiwa. Hivi ndivyo aliyotutumia jumbe:


Nimekuwa nikisoma mashapisho ya Nesi Mapenzi kwa muda wa miezi mitatu sasa na naweza kusema nimenufaika sana na maujanja yenu ambayo mnayaandika bure watu kuyasoma.
.
Wiki kadhaa zilizopita nilipata kuisoma hii mbinu ya majukumu mjeuko na mpaka sasa nimefaulu kudeti wanawake watatu (wawili niliwapata kwa supermarket na mmoja nilimnasa kwa klabu)
.
Nilikuwa na uliza kama kunaweza kuwa na mbinu ya kumkiss mwanamke? Yaani mbinu ya kumfanya yeye aanzishe kiss? Naweza kupata ujanja kuu kwangu na maelfu ya wengine kama mimi?
Shukrani za dhati ziwafikie.- Joni, Mwanza (via email)
Ok hatujashangazwa kuwa mbinu ya majukumu mjeuko ilifanya kazi nzuri kwako - kwa kawaida mbinu tunazoziweka hapa huwa zimefanyiwa utafiti kwanza ndipo iidhinishwe na admin.

Sasa kwa kuwa umepata deti kirahisi, utakumbwa na changamoto mpya na tofauti kabisa, hio si bila shaka ;)

Ushawahi kujaribu kwenda katika deti ambazo zinaonekana kudumu milele bila kuendelea kujeuka kuwa romantiki? Si wewe pekeako, ndugu.

Wanaume wengi wanajua jinsi ya kufanikisha deti, lakini wanaanguka kufanya deti yao isisahaulike kwa kuimalizia na kiss.

Unafaa kuelewa ya kuwa jambo gumu la kufahamu wakati unapokuwa na mwanamke ni wakati mwafaka wa kumkiss.

Kumuuliza kabla hajakuwa tayari unaweza kujitakia akukatae, na pia kukawia sana kutamaanisha kukosa ule wakati 'spesho'

Kila kiss inapaswa kuwa timilifu, lakini kiss ya kwanza inapaswa kuwa isiosahaulika.

Hii hapa ni mbinu ambayo itakufanya upandishe gemu yako ya kukiss wakati umetoka deti na mwanamke.

Hii inapaswa kujaribiwa na mwanaume yeyote yule, so endelea kusoma.

Baada ya kusoma hii post utagundua ya kuwa kutaka kukiss girl friend wako ama katika deti si jambo gumu kama utamruhusu yeye akubusu wa kwanza.

(So kumjibu Joni ni kuwa NDIO, mbinu hii ipo ya kumfanya mwanamke aanzishe kiss)

Najua ushawahi kuskia mahali ile mbinu ya hisia mkato ambayo unajizuia ili ujenge tenshen zaidi, lakini pia unahitajika kumwanzisha mwanamke na kumkontrol utangamano wenu ili umfanye atake kukukiss hapo hapo bila kumuomba moja kwa moja.

Zama nami!




Hatua #1: Mpeleke sehemu ya faragha
Hii haimaanishi kumtoa katika klabu aliyokuwemo, kwa sababu anaweza kukataa kuacha marafiki zake nyuma.
Unaweza kuenda katika sehemu iliyotengwa pembeni ambapo mnaweza kuongea sirini bila kutatizwa. Ama mnaweza kujitenga pamoja (kama mko katika kikundi kikubwa) kwa kumuuliza aandamane na wewe katika baa ama sehemu nyingine kando na hio klabu .
Hatua #2: Hakikisha yuko shwari kuongea, kubanta na wewe kabla hujaendelea zaidi
Kwanza ruhusu dakika chache za kuongea na kujiskia huru kabla ya kuvunja utangamano wenu kwa kujenga tenshen ya mapenzi.
Jambo la mwisho ambalo unataka kwake ni kuona akijutia busu lako, hivyo hakikisha kwanza kuwa anainjoy company yako kabla hujakimbilia hatua yeyote ya ziada.

Hatua #3: Wakati anazungumza kuhusu hoja isio na msingi ama akiwa ana banta, unawezakuangalia upande aliko na umkate katikati ya sentensi.
Mwambie "Kusema kweli ni kuwa simakiniki na mada unayoizungumza. Kile ambacho nafikiria sahizi ni kukubusu."

Anaweza kushikwa na haya, kunyamaza ama kutojiskia huru, lakini ufunguo hapa ni kuendeleza na maneno haya: " Lakini SITAKI kukukiss kwa sasa kwa sababu unaonekana hauko tayari kwa busu la hakika. Kile ambacho tutafanya ni kufanya mazoezi ya kukiss."

Hatua 4: Pindi utakapo mwambia, mwonyeshe vile inapaswa kufanywa.
Mwambie kuwa atulie na asiingiwe na wasiwasi kuhusu kukuss kwa sababu hautambusu. Mwanzo muahidi kuwa hutamkiss na pia yeye atoe ahadi yake.

Hii ni hatua muhimu - hivyo makinika!

Wakati umeshatoa ahadi yako, mwekee mikono yako kwake na umsogelee pole pole.

Unaweza kuongea na yeye kwa upole lakini uwe unamsogelea karibu hadi midomo yenu iko karibu kugusana halafu pole pole unajisogeza mbali.

Hatua #6: Muulize "Si imekuwa furaha?"
Nafasi kuu hapa ni kuwa umemchangamsha na atataka ujaribu tena.
Kama hakuchangamshwa, unaweza kumuuliza tena mjaribu tena zoezi la kikiss (bila kumkiss kiukweli). Kufikia huu wakati, tenshen itakuwa imejijenga na kila wakati utakapofanya 'zoezi' la kumkiss, ndivyo atazidi kutamani umkiss kiukweli.

Hatua #6: Kama atakukiss, jiachilie umkiss kwa dakika chache halafu kiulaini jivute nyuma na useme haya maneno kidhihaka "ok, imetosha mvunja ahadi"

Baada ya hapo unaweza kubadilisha mada na kuongea mambo mengine, kana kwamba hakuna kitu kilichotokea.


Hatua #7: Baada ya muda, unaweza kujaribu kumuuliza yeye ajaribu tena kufanya mazoezi ya kukiss. Kama wakati uliopita, mwambie akuhakikishie ya kuwa hatakukiss. Mfanye kama alivyofanya awali.

Kufanya hivi mara zaidi kutafikia yeye kukukiss tena, wakati huu ikiwa na ashki zaidi.

So wakati mwingine ukiwa unajiskia kumkiss mwanamke lakini unatatizika fuata hatua hizi saba - na anaweza kukukiss wa kwanza!