Thursday 18 August 2016

Mkurugenzi wa ‪#‎CloudsMediaGroup‬, @josephkusaga atembelea WCB Cheki tukio zima hapa

Mkurugenzi wa ‪#‎CloudsMediaGroup‬, @josephkusaga atembelea WCB
‘’Ni muda mrefu tumekuwa tumeongea na @diamondplatnumz na timu yake, Babu Tale na Salaam mimi kupata nafasi ya kwenda kuwatembelea kuangalia shughuli wanazozifanya lakini kutokana na ufinyu wa ratiba zangu imekuwa ngumu lakini jana niliwatembelea na kuona jinsi watu ambao nimefanya nao kazi kwa miaka mingi kwa roho safi wanavyofanya kazi, kiukweli Diamond na timu yake jana nimeona kitu wanachokifanya ambacho watanzania wengi inabidi watoe sapoti kubwa sana kwake, kwanza utaratibu mzima wa shughuli alizozipanga na pili sapoti kubwa sana ya vijana ambayo anaifanya na sisi tulivyoanza ilikuwa hivyo hivyo tu, watu wawili au watatu lakini sasa hivi tunaona jinsi ilivyokuwa, hata yeye miaka miwili ambayo amefanya shughuli zake lakini kuna vijana wengi ambao wanapata ajira hapo WCB, napongeza sana