Tuesday 16 August 2016

JE MWANAMKE UNA UKOSEFU WA HAMU YA KUFANYA MAPENZI (LOW LIBIDO IN WOMEN) NA MAUMIVU WAKATI WA TENDO LA NDOA LA NDOA?..SULUHISHO LAKE HILI HAPA

Habari za leo ndugu msomaji wa blog hii ni matumaini yangu unaendelea vizuri na kufurahia blog yangu,
Leo nimependa kuzungumzia tatizo la ukosefu wa hamu ya kufanya tendo la ndoa ambalo ni changamoto kubwa katika ndoa za walio wengi na Hali hii imekua na athari kubwa katika familia zetu
LOW LIBIDO IN WOMEN (UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIKE)_ni hali ya ukosefu wa hamu ya kufanya mapenzi kwa mwanamke, tatizo hili hutokana na sababu tofauti mfano uwiano mbaya wa homoni nk, wanawake wengi nchini na Duniani wanasumbuliwa na tatizo hili la kutopata hamu ya kufanya tendo la ndoa na kushindwa kufika Kileleni, inasadikika kuwa katika kila wanawake kumi basi wanne Kati yao Wana tatizo hili.
~Mara nyingi ugonjwa huu husababishwa na mambo makuu mawili ambayo ni matatizo ya kimwili na matatizo ya kisaikolojia
1)MATATIZO YA KIMWILI (PHYSICAL)
kuna magonjwa mengi yanayosababisha tatizo hili baadhi ya magonjwa hayo ni ANEMIA(UPUNGUFU WA SELI HAI NYEKUNDU ZA DAMU) ugonjwa huu ni chanzo KIKUU cha tatizo hili kwasababu huambatana na upungufu wa madini ya chuma (iron) ambayo ndio hufanya kazi ya kusisimua mwili na kuongeza hamu ya tendo la ndoa, Mara nying wanawake wanapokua katika hedhi huwa wanapoteza kiwango kikubwa cha madini ya iron ambayo hutolewa mwilini kupitia damu hvyo huchangia asilmia kubwa kupoteza hamu ya kufanya tendo la ndoa, pia mabadiliko ya homoni katika mwili huwa ni tatizo kubwa kwasababu mwanamke anapokua katika Hali ya kawaida uzalishaji homoni huwa ni wa kawaida ila atakapo kua ananyonyesha au mjamzito mwili huzalisha LUTEINISING HORMONE (LH) ambayo huondoa hamu ya kufanya tendo la ndoa
2)SABABU ZA KISAIKOLOJIA
sababu hizi hutokana na mazingira na vipindi tunavyopitia hivyo kuwa hatarishi kwetu na kuwa chanzo cha kupata tatizo la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa yafuatayo ndio Vyanzo vya tatizo hili
~Msongo wa mawazo
~woga
~mazingira magumu
~manyanyaso ya jinsia au kubakwa wakati wa utoto
~huzuni
~kumbukumbu mbaya kichwani nk
MATIBABU NA JINSI YA KUJIKINGA NA UGONJWA HUU
matibabu ya ugonjwa huu hupatikana kwa ugumu kidogo na hufanyika na kutolewa kupitia vipimo vya uchunguzi, historia ya mhusika pamoja na Dalili za magonjwa mbalimbali pia pamoja na hayo tatizo hili unaweza kulitibu kwa kuzingatia yafuatayo
👉EPUKA KUVUTA SIGARA
👉ZINGATIA ULAJI MZURI KWA AFYA YAKO
👉ONDOA MAWAZO NA HUZUNI
👉ONGEZA MSISIMKO KATIKA MAHUSIANO YAKO
👉ACHA ULEVI
👉BADILISHA MFUMO WA MAISHA YAKO
👉WEKA MAZINGIRA MAZURI NA MUDA WA KUFANYA TENDO LA NDOA

JE UNAFAHAMU NINI KUHUSU SOY???
Maharage ya soya ni miongoni mwa vyakula maarufu nchini mwetu pia nchini China zao hili ni la thamani sana na limekua sehem ya mlo kamili kwa wananchi wake kwasababu soy Ina faida nyingi za kiafya kutokana na kuwa na kiwango kikubwa cha protein, pia soy Ina kiwango kidogo cha fat na pia Zina PHYTOESTROGENS ambayo husaidia sana wanawake walioko katika menopause hutengeneza homoni ya estrogen ya Ziada pia husaidia uke kuwa laini (WET, LUBRICATED) ambavyo pia huongeza stamina na hivyo kuwa na hamu ya kufanya tendo la ndoa Mbali na hvyo pia soy Ina vitamin vingi A, B complex C, D, E, F, G, H, na K pia soy Ina glycerin na faty acid ambayo husaidia ufanyaji kazi wa ubongo na maini pia mafuta ya SOY yanapotumika kupakwa kichwani huondoa MBA na ukurutu