Tuesday 16 August 2016

HILI NDILO SULUHISHO LA FANGASI UKENI,SOMA ZAIDI HAPA

UGONJWA WA FANGASI UKENI (VAGINAL CANDIDIASIS)
Habari za leo ndugu msomaji wa blog hii, leo napenda kuzungumzia ugonjwa huu wa fangasi kwa wakina mama na Dada ambao umekua common na kuwatesa,
_maambukizi ya fangasi sehemu za siri imekua tatizo kubwa sana Duniani 75%ya wanawake wote Duniani wanasumbuliwa na tatizo hili
_maambukizi ya fangasi katika sehemu za siri za mwanamke husababishwa na fangasi wanaoitwa CANDIDA ALBICANS, maambukizi haya pia hujulikana kama YEAST INFECTIONS /THRUSH
_CANDIDA ALBICANS hupatikana katika midomo,mpira wa kupitishia Chakula (PHARYNX), kibofu cha mkojo, uume au katika uke
_bacteria Hawa huishi katika sehemu hizo Bila kuleta madhara, isipokua pale mazingira ya eneo husika yanayojadiliwa, MFANO mabadiliko katika Hali ya PH, kwa kawaida PH ya mwanamke ndani ya uke ni 4.0_4.5 au uwiano wake na vimelea 3.8_4.2 (microorganisms) wengine, hivyo huharibiwa kutokana na sababu mbalimbali kama vile matumizi ya MADAWA ya antibiotics eg AMPICILLINE, CIPROFLAXINE, AMOXYLINE, DOXYCYCLINE, ERTHROMYCINE, NK, pia kupungua kwa Kinga kutokana na magonjwa tofauti,NK
_Maambukizi ya fangasi ukeni yamegawanyika katika sehemu KUU mbili
A) MAAMBUKIZI YASIYO MAKALI (UNCOMPLICATED THRUSH)
Katika aina hii mgonjwa hupatwa na maambukizi Mara moja hadi nne kwa mwaka pia Dalili zake huwa si za kuogopesha na maambukizi haya husababishwa na fangasi aina ya CANDIDA ALBICANS
B) MAAMBUKIZI MAKALI (COMPLICATED THRUSH)
Katika kundi hili mgonjwa hupatwa na maambukizi Zaidi ya Mara nne au Zaidi kwa mwaka pia Dalili zake huwa ni za kuogopesha kama maambukizi yatakua yametokea kipindi cha UJAUZITO, ugonjwa wa VVU, ugonjwa wa sukari nk
VIHATARISHI VYA MAAMBUKIZI YA FANGASI KATIKA UKE
Vihatarishi vya maambukizi ya fangasi ukeni ni mengi sana ambayo ni pamoja na mabadiliko ya mfumo wa homoni mwilini ambao husababisha mabadiliko katika sehemu za siri pia Vihatarishi vingine ni hivi 👇
@saratani ya tezi koo (thyroid cancer)
@msongo wa mawazo
@utapiamlo (malnutrition)
@matibabu ya homoni(hormonal replacement therapy)
@ujauzito
@kujamiiana kwa njia ya haja kubwa (anal sex
@matumizi ya glycerin wakati wa kujamiiana
@kuvaa nguo au mavazi yanayoleta joto
@matumizi ya dawa za Uzazi wa mpango
DALILI ZA UGONJWA
WA FANGASI UKENI
👉kuwashwa sehemu za siri
👉kuhisi maumivu wakati wa tendo la ndoa(superficial dysapareunia)
👉kuhisi kuwaka moto sehemu za siri (burning sensation)
👉kupata vidonda au michubuko ukeni (soreness)
👉kuvimba na kuwa mwekundu katika mdomo wa nnje wa uke (Labia minora
👉kupata maumivu wakati wa kukojoa
👉kutokwa na uchafu wa rangi nyeupe au kijivu unaoweza kuwa mzito, mwepesi au majimaji
NOTED : DALILI HIZI HUWA MBAYA ZAIDI WAKATI WA BLEED
MATIBABU NA JINSI YA KUJIKINGA NA UGONJWA HUU WA FANGASI UKENI
Ugonjwa huu wa fangasi matibabu yake hupatikana kwa urahisi Tanzania na tiba hupatikana na kutolewa kupitia vipimo vya uchunguzi na majibu yaliyotoka, pamoja na hayo ugonjwa huu unazuilika hivyo njia nzuri ni kujikinga kwa kufanya yafuatayo
👉Vaa chupi ambazo hazibani na zilizotengenezwa kwa pamba au hariri epuka synthetic underwear
👉Epuka kufanya mapenzi na mpenzi wako mwenye maambukizi haya
👉KULA mlo wenye virutubsho
👉Epuka kuoga maji ya moto (hot baths) kipindi cha joto tumia maji ya vuguvugu
👉osha sehemu zako za siri kwa kutumia maji Safi na sabuni ya asili inayoitwa lady intimate wash na tumia kitambaa kisafi kujikausha maji
👉epuka matumizi ya vifaa vya kufanyia mapenzi (sex toys)au vifaa vya kupanga Uzazi (diaphragm cervical caps) husababisha maambukizi ya fangasi
👉tumia pads na pantiliner zenye anions zinazoitwa NEPLILY
👉kunywa maziwa aina ya mtindi yenye live culture Mara kwa Mara kwani husaidia kuepusha maambukizi haya
👉epuka kutumia sabuni zenye manukato kama vile Bath powder, feminine hygiene, bubble baths, vaginal deodorant