Tuesday 14 October 2014

Uliwahi kuipata hii kuhusu kufungwa kwa magereza nchini Nertherlands?

Screen Shot 2014-10-13 at 10.55.50 AMUnaambiwa mwaka 2009 nchi ya Netherlands iliamua kufunga magereza yake tisa kutokana na upungufu wa uhalifu nchini humo ambapo mpaka mwaka 2013 jumla yamagereza
19 yalifungwa kutokana na kuzidi kupungua kwa uhalifu nchini humo.
Screen Shot 2014-10-13 at 10.54.55 AM
Upande wa kushoto ni gereza mojawapo la Netherlands ambalo limebadilishwa kuwa Hotel (Kulia).
Kingine cha kufahamu ni kwamba watuhumiwa hupewa nafasi ya kuchagua adhabu ya kwenda jela au kutokwenda jela lakini mienendo yao hufuatiliwa kwa kuangaliwa simu zao, computer, magari n.k yaani chochote unachofanya kinaonekana (Electronic tagging).
Ambapo asilimia kubwa ya watuhumiwa hao huchagua adhabu hiyo ya Electronic taggingna kurudi uraiani kufanya kazi kama kawaida.
Screen Shot 2014-10-13 at 10.55.19 AM
Hili ni gereza mojawapo la Netherlands linaitwa David Leventi Breda
Serikali ya Nerthelands inasema kufungwa kwa magereza haya kumesaidia kuokoa dola za Kimarekani elfu hamsini ($50,000) ambazo kwa Tanzania ni zaidi milioni 80 ambapo watuhumiwa wenye makosa madogo yanayofanyika kwenye kata mbalimbali na nchi nzima hupewa adhabu ndogondogo kama kufanya kazi za kijamii.
Sasa hivi nchi hii ambayo rekodi za mwaka 2013 zilionyesha ina watu milioni 16.8 inajaribu kupunguza ukiukaji wa amri na uvunjaji wa sheria kwa kuwapeleka watuhumiwa kwenye vituo maalum vya kurekebisha tabia. (Rehabilitation Centers).