Sunday 19 October 2014

AUNTY LULU AMPA SOMO JOHARI

SOMO! Staa wa Bongo Movies, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ ameibuka na kumtaka msanii mwenzake, Blandina Chagula ‘Johari’ kukubaliana na matokeo ya aliyekuwa mpenzi wake Vincent Kigos ‘Ray’ kwamba kwa sasa
ana uhusiano na mtu mwingine.
Staa wa Bongo Movies, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’.
Akistorisha na paparazi wetu, Aunty Lulu alimtaka Johari kukubaliana na matokeo na aige mfano wake kwani aliachana na Bond Bin Sinan ambaye kwa sasa ana mpenzi mwingine hivyo asimchukie Chuchu Hans anayetoka na Ray kwa sasa kwani kuachana ni jambo la kawaida katika mapenzi hivyo hatakiwi kuwa na kinyongo.
Msanii Bongo Movies, Blandina Chagula ‘Johari’.
“Mimi nimepitia kwenye maisha hayo ndiyo maana namshauri Johari akubaliane na matokeo kwamba Ray kwa sasa yupo na Chuchu Hans na asiwe na kinyongo naye ampende na aongee naye vizuri tu kwani ndiyo maisha,” alisema Aunty Lulu.