Wednesday 22 October 2014

''MPENZI WANGU ANANISALITI KWA WANAWAKE WEMBAMBA,SASA SIJUI MIMI ALINITAKA WA NINI?

MIMI ni msichana mwenye umri wa miaka 23 naitwa Samantha wengi hunitania na kuniita Bonge, elimu yangu sio mbaya sana na nimtoto wa familia yenye maisha mazuri kias fulani,

Nimekuwa nikiteswa na mfumo wa mapenzi yetu mimi na mpenzi wangu maana nashangaa tangu tuanze mahusiano nimemfumania zaidi ya mara 4 na
mimi bado nampenda jamani kibaya zaidi wanawake wote naomnasa nao ni wembamba kama njiti, Sasa sielewi kama alikuwa anapenda wanawake wembamba kwanini anitongoze? Alafu ukizingatia huyo mpenzi wangu ni mwembamba mrefu inamaana haoni kama tunaendana?..

Na mimi natongozwa sana na mkaka mmoja hivi tupo nae kazini kwangu nafanya nae kazi ofisi moja yeye ni mesenja Sijui nimkubalie ili ngoma iwe droo? Naombeni ushauri jamani maana Admin amaniambia niwaombe nyinyi ushauri yeye hana la kusema.