Saturday 14 March 2015

MWANAMKE ANAHITAJI NINI KUTOKA KWA MWANAUME? KAMA NI MAPENZI YANATAKA ELIMU

alama na hivyo kuyafanya mapenzi yao kudumu kwa muda mrefu. Wanaume wa siku hizi wamekuwa hawafahamu ni vitu gani ambavyo wanawake wanapenda kuvipata kutoka kwao.

Kushindwa kuwa na elimu hii, wanaume wengi wamejikuta wakitumia ukali kuwatawala wake zao, jambo ambalo limekuwa likizidisha migogoro ya kimapenzi na hatimaye wapenzi huachana. Yafuatayo ni mambo muhimu ambayo wanawake hupenda watendewe na wapenzi wao.


KUTATULIWA MATATIZO
Wanawake wengi hutegemea kuwa wanapokuwa na wapenzi watasaidiwa katika matatizo ya kimaisha na migogoro ya kimawazo. Kwa mfano ushauri juu ya maisha yao, kulindwa na hatari za kimaisha, kusaidiwa katika shida na kuongozwa pale wanapohisi kushindwa kufanya jambo. Kama mwanaume hatamfanyia mpenzi wake hili atakuwa amekosa sifa za kuteka penzi la mwanamke.

KUBEMBELEZWAWanawake hupenda kubembelezwa pale wanapokuwa na huzuni, wengi wao hawapendi kukaripiwa, mara nyingi hupenda kuungwa mkono wanapokuwa na misuguano na wengine. Ili mwanaume amteke kimapenzi mwanamke lazima awe nyuma yake hata kama atakuwa na kosa. Wanawake wengi hupenda kuelimishwa zaidi kuliko kufokewa.

KUWA NAMBA MOJA Safari ya penzi la mwanamke haishii kwenye kumpata na kumliki, kisha kujisahau kwa kisingizio kuwa umemuoa au umemvisha pete ya uchumba, ni zaidi ya hapo. Jambo la tatu ambalo wanawake wengi huhitaji ni kuwa namba moja au kupendwa. 
Wanapenda watangulizwe katika mapenzi na kusiwepo na mwingine wa kuchukua nafasi yao katika mazungumzo na mapenzi kwa ujumla. Wanawake hawapendi kuitwa majina mabaya kwa mfano mjinga, Malaya au kulinganishwa na wanawake wenzao wabaya.

KURIDHISHWA KWENYE TENDO Hata kama utakuwa na kiwango kikubwa cha mapenzi juu ya mpenzi wako kwa kiwango gani, ukiwa dhaifu katika tendo la ndoa utayumbisha penzi lako. Ni wajibu wa mwanaume kuhakikisha kuwa anamtosheleza mpenzi wake katika tendo hilo. Utundu unahitajika ili kumkata kiu mpenzi wako.

MAZUNGUMZOWanawake wanatajwa kuzungumza maneno 25,000 kwa siku, huku wanaume wakibaki na kiwango cha maneno 5,000 kwa siku, hii ikiwa na maana kuwa wanawake hupenda zaidi kujieleza walivyo mbele ya wengine. Kwa msingi huo wakizuiwa wasiongee hujiona kama wanakosa nafasi muhimu ya kueleza mawazo yao. Kama una mpenzi wako mpe uhuru wa kuzungumza na kumsikiliza bila kumkatiza kwa ukali.