Thursday 25 December 2014

UNAAMBIWA MISS WORLD YAFUTA KILE KIPENGELE CHA VAZI LA UFUKWENI


Miss World imeamua kufuta kipengele cha vazi la ufukweni.
Miss World imeamua kufuta kipengele cha vazi la ufukweni.
Waandaaji wa mashindano ya urembo ya dunia maarufu kama Miss World wamefuta sehemu ya shindano hilo inayohusisha warembo wakiwa wamevalia nguo za kuogelea maarufu kama vazi la ufukweni au Beach Wear.
Mkurugenzi wa mashindano haya Chris Wilmer amesema kuwa sababu ya kfuutwa kwa kipengele cha mashindano ya cha nguo ya kuogelea ni kushindwa kuendana na vipengele vingine vya mashindano haya .
Mkurugenzi huyo amesema kuwa mashindano haya pamoja na kuwa mashindano ya urembo lakini hayahusishi urembo pekee bali urembo na sababu maalum na hakukuwa na sababu yoyote maalum ya kujumuisha kipengele cha nguo za kuogelea .
miss worldd
Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa Mshindi wa Miss World anapaswa kuwa balozi na msemaji wa jamii ya watu sio malkia wa urembo pekee .
Maadili na kile anachowakilisha mshindi wa Miss World ndio kinachotazamwa kwa mshindi hivyo kwa sababu hiyo Miss World haitakuwa na kipengele cha shindano la nguo ya kuogelea .
Kipengele hiki kimekuwepo tangu mwaka 2001 wakati kilipopewa jina Beach Fashion huku kikifanywa kama  kipengele binafsi ndani ya shindano hilo