Thursday 18 December 2014

RAIS WA SERIKALI YA WANAFUNZI UDOM ATOA SABABU ZA WANAFUNZI HAO KUJIUZA

Rais wa Serikali ya wanafunzi chuo kikuu cha UDOM Masatu Kyabwene amekiri kuwepo kwa idadi kubwa ya wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu Dodoma kujihusisha na biashara ya ukahaba kutokana na kukosa mikopo.


“Kuna baadhi ya wanafunzi chuoni kwangu wana maisha magumu sana kutokana na kukosa mkopo,wakati mwingine wananifuata mimi na kunielezea shida zao ili niwasaidie,wengine ni yatima hawana baba wala mama wa kuwalipia ada,siyo siri maisha ya wanafunzi hawa ni magumu sana”amesema.