Thursday 6 November 2014

Story kamili kuhusu Nicki Minaj na Boyfriend wake

safaree-samuel-and-nicki-minaj-nicki-minaj-1dvlgq1Hivi karibuni Femcee anayetesa kwenye anga za Rap nchini Marekani Nicki Minaj anayeitendea haki vilivyo label ya YMCMB alitangazwa kuachana na ‘Boyfriend’ wake wa zaidi ya Miaka kumi anayefahamika kwa jina la Safaree Samuels.

Kuachana kwa wawili hawa kumetangazwa sana kwenye mitandao na magazeti pamoja na vyanzo tofauti vya media ulimwengu mzima lakini haijawahi kufahamika wazi nini hasa chanzo cha wandani hawa kuamua kuupiga stop uhusiano wao .
Safaree Samuels akionekana na tatoo yenye sura ya Nicki Minaj na Jina lake kifuani.
Safaree Samuels akionekana na tatoo yenye sura ya Nicki Minaj na Jina lake kifuani.
Imefahamika kuwa chanzo cha wapenzi hawa kuachana ni kitendo cha Nicki Minaj kumletea jamaa wake ‘swagger’ za kimtaa kimtaa baada ya kugundua kuwa ana nyendo tofauti na madem wengine .
Stori ni kuwa Nicki kuwa alichukua gongo linalotumika kwenye mchezo wa baseball maarufu kama ‘Baseball Bat’ na kumfukuza Safaree akimkimbiza kutoka nyumbani kwake .
Nicki Minaj ambaye alivunja gari ya Boyfriend wake Safaree Samuels.
Nicki Minaj ambaye alivunja gari ya Boyfriend wake Safaree Samuels.
Kana kwamba hiyo haitoshi; Nicki aliingia kwenye sehemu ya kupaki magari ambako alimalizia hasira zake kwenye gari ya kifahari ya jamaa huyo aina ya Mercedez Benz ambapo aliishambulia kwa nguvu zake zote na kuiharibu.
Baada ya hapo wapenzi hawa wameachana na hakuna dalili zozote za kurudiana japo huwezi jua , chochote kinaweza kutokea.