Sunday 2 November 2014

MWANAFUNZI WA CHUO ANAYESOMEA UPADRI ANASWA AKICHEPUKA NA MKE WA MTU HUKO MORO GORO


Bw. Leonard Celestine aliyeaibika gesti na mke wa mtu. 

Aibu kuu! Jamaa aliyejitambulisha kwa jina la Leonard Celestine ambaye anasomea upadri, anayemalizia masomo ya falsafa (philosophy) mwaka wa tatu katika Chuo cha Jordan mjini Morogoro, anadaiwa kuaibika gesti, kisa kikiwa ni mke wa mtu gesti.


TUJIUNGE GESTI
Kwa mujibu wa shuhuda wetu, tukio hilo la aina yake lilijiri hivi karibuni kwenye Gesti ya Silver Inn iliyopo maeneo ya Msamvu mjini Morogoro ambapo kijana huyo alipewa kipondo cha aina yake na kunyang’anywa kila kitu huku akiachwa kama alivyozaliwa na kulazimika kujisitiri na taulo la nyumba hiyo ya wageni.
KITU LAIVU!
Chanzo hicho kilidai kwamba, kijana huyo ambaye ni mwenyeji wa Iringa alikuwa na mchezo wa kutembea na huyo mke wa mtu tangu mwaka jana ambapo mumewe aliamua kumwekea mtego ulipofyatuka akanaswa laivu.
Bw. Leonard Celestine akijutia soo lililomkuta.
KUMBE!
Ilidaiwa kwamba, kama ilivyo seminari zote za Kikatoliki, mwanafunzi hutakiwa kukaa ndani lakini Leonard alidaiwa kuwa alikuwa akitoroka hasa siku za wikiendi au siku akiwa na vipindi vinavyoishia asubuhi na kwenda kukutana na mke huyo wa mtu na kujiachia naye kwani mumewe ni mtu wa kusafiri mikoani.
Ilisemekana kuwa kutokana na kujiachia huko mwenye mke aligundua na kuanza kumfuatilia tangu mwaka jana hadi alipowanasa hivi karibuni.

KIPIGO
Baada ya kunaswa, Leonard alipewa kipigo cha aina yake na watu ambao tayari walikuwa wameshaandaliwa na mwenye ‘mali’ ambapo alilia huku akiomba asamehewe ili yasije kuvuja akakosa upadri kwani ameshafika mbali.
Bw. Leonard Celestine akibanwa kwa maswali mara baada ya kupewa taulo kujisitiri.
APOKONYWA KILA KITU
Ilidaiwa kwamba, raia hao wenye hasira walimpokonya simu, begi lake lililokuwa na madaftari na nguo hivyo alitoka chumbani bila nguo na badala yake aliomba taulo kujisitiri.

PADRI ANASEMAJE?
Gazeti hili lilimtafuta Leonard kwa njia ya simu aliposomewa mashtaka yake alisema:


“Ni kweli hizo picha ni zangu, nalijua hilo tukio lakini ndugu mwandishi naomba usinitoe, nitakuwa nimekwisha kwani yule mwanamke hakuniambia kama ni mke wa mtu.”