Thursday 21 July 2016

Picha: The Game alivyo amua kumsaidia Mama mwenye watoto nane

Rapper The Game hivi karibuni kupitia kampeni yake ya “Yo Mama, My Mama”, anaendelea kutoa misaada tofauti kwa jamii iliyomzunguka rapper huyu kutoka Compton, California alitumia dola $1,000 kununua vyakula vya familia ya mama mwenye watoto nane.


Mama huyu ambaye anaitwa Yvette Hicks ana watoto nane na ameachana na mume wake, hivi karibuni mtoto wake wa kike Eunice alirekodi video na kuiweka katika mtandao huku akitoa sababu za kwanini mama yake ana haki ya kupata msaada huo na ndipo The Game aliiyona na aliwatembelea na kuwapa msaada huo.