Thursday 21 July 2016

Lulu kajibu swali kuhusu ile pete aliyoipost Instagram akiwa kaivaa

Mwigizaji wa bongo movie Elizabeth Michael ‘Lulu’ alizichukua headlines kwa kupost picha akiwa kavaa pete ya uchumba na kuandika >>> ‘Asante Mungu wangu kwa neema zako ambazo hazijawahi kuniacha, maana hata hiki kitendo cha kishujaa kujinunulia pete nzuri kama hii ni kwa neema tu‘

Ni swali ambalo wanaofatilia maisha ya Lulu wamekua wakijiuliza mpaka leo na wengine wanahisi ni kweli alivishwa pete ya uchumba lakini akaamua kuileta kwa namna hiyo ambapo hata hivyo aliifuta post hiyo muda mfupi baadae.
Lulu amesema ‘Sikuwa na sababu maalum za kuiweka na kuifuta, nilikua nacheza tu na nimekuja kugundua Watanzania wanapenda sana drama, nilivyoona comments ndio nikajua ni watu wa aina gani wananifatilia, ni pete ambayo niliinunua nikaivaa’