Friday 18 November 2016

Gabo auzungumzia umuhimu wa tuzo za EATV Award pamoja na mwamko mdogo wa mastaa

Msanii wa filamu anayefanya vizuri na filamu ‘Safari ya Gwalu’ Salim Ahmed ‘Gabo’ amesema tuzo ni kitu muhimu kwa wasanii kwa kuwa ni kipimo ambacho kinapima mafanikio ya msanii husika.
Gabo

Muigizaji huyo ambaye anawania tuzo ya muigizaji bora wa kiume katika tuzo za EATV Award, amesema hatua ya kuongezeka kwa tuzo nchini kunasaidia kukuza sanaa.

“Tuzo ni kitu kikubwa sana kwa upande wa wasanii kwa sababu nchi za wenzetu wanatuzo nyingi ambazo zinawafanya wajione wako juu au wanafanya vizuri,” alisema Gabo. “Tuzo ni kama kipimo cha mtu baada ya kufanya kazi, kwahiyo mimi niwashukuru sana EATV kwa kututeletea tuzo,”

Kwa upande wa ufinyu wa mastaa waliojitokeza, Gabo alisema “Lakini nikirudi kwa walioandaliwa tuzo kuna uzito kidogo kwa waliojitokeza, watu wameshindwa kuamka na kuona chakwetu tukichangamkie lakini kwao imekuwa ngumu,”

Pia muigizaji huyo alisema huwenda ugeni wa tuzo hizo ndio kitu kingine kilichofanya mastaa wengi kutokuwa na mwamko zaidi.