Thursday 30 April 2015

Epuka mawazo hasi kwa mwenzi wako, ni ugonjwa wa moyo



Taarifa kwako msomaji wangu ni kuwa kuna watu wengi wameachana kwa sababu ya kuwa na mawazo hasi juu ya wenzi wao. Hakuna imani kati yao.Iwe mmoja anamtuhumu mwenzake au wote ni kama Pwagu na Pwaguzi.Zipo hisia zinazowaongoza wanaume wengi kuhusu wanawake. Hawataki wafanye kazi,
ikibidi wakae tu nyumbani kwa hoja kuwa wanapokuwa maofisini wataanzisha uhusiano mpya na wafanyakazi wenzao au kwenye mapito ya kazi zao.Wale wanaoruhusu wake zao wafanye kazi, kila siku roho juu. Macho pima kwenye simu za wenzi wao. Hawana imani ya asilimia 100 kwamba siku hupita bila kusalitiwa. Wanateswa na sononeko la moyo. Pengine mwenzake ni mwaminifu lakini wasiwasi wa mapenzi ndiyo ugonjwa wa moyoHaipendezi kumfikiria mwenzako kwa ubaya. Inashauriwa umuamini na ujiamini. Mawazo chakavu kuhusu mwenzi wako ni sumu. Ukiyaendekeza yanaweza kukufanya ushindwe kutekeleza mambo ya msingi.Mwanamuziki Stara Thomas amelifafanua hilo vizuri kwenye wimbo wake wa Wasiwasi wa Mapenzi. Kwamba mtu anaweza kujawa na hofu ya kusalitiwa na mwenzi wake mpaka roho ikawa juu juu. Kumbe siyo kweli hata kidogo.Unaweza kumvaa mtu asiye na hatia na kugombana naye kwa sababu tu ya mawazo kwamba anakuchukulia mali yako. Siku zinasogea, baadaye unakuja kugundua kuwa hisia ndizo zilikupeleka ndivyo sivyo.Busara za kisaikolojia zinakutaka uwe huru, kwa maana unatakiwa ujiepushe na mawazo mabaya. Mtu akipiga simu ya mwenzi wako, usikurupuke na kuanzisha songombingo, hebu vaa utulivu na upate ufumbuzi kwa njia yenye nidhamu.Kushika simu ya mwenzi wako na kukagua simu zinazoingia na kutoka ni alama ya kutoamuamini.Ingekuwa humtilii shaka yoyote, usingethubutu kukiganda ‘kiselula’ chake. Hujui tu, unamdhalilisha kwa kumuona hajatulia.Unataka kuona SMS zinazoingia na kutoka. Hulali mpaka uone simu alizopiga na alizopigiwa. Presha hiyo yote ya nini? Jaribu kumuamini na umuoneshe jinsi usivyo na shaka naye. Mwache yeye mwenyewe atumie vibaya imani yako kwake.Kuna mtu kwa wasiwasi alikuwa anashindwa kutimiza majukumu yake ya kila siku, badala yake anakwenda kujificha nje ya ofisi yamke wake, anashinda pale, lengo ni kuona wakati wa ‘lunch’ mkewe anaongozana na nani.Ikiwa siku hiyo mkewe kaongozana na mfanyakazi mwenzake wa kiume kwenda lunch, jioni nyumbani ni kesi. “Nimepata taarifa zako, leo ulikwenda lunch na mwanaume, yule ni nani?” Hana lolote, hajaambiwa na yeyote, ni yeye mwenyewe na upekupeku wake.UNAMKOSEA HESHIMA MWENZI WAKOIwe hutaki mwenzi wako afanye kazi au unamsumbua kwa namna yoyote ile, jawabu ni moja tu kwamba humheshimu. Kutokuwa na imani na yeye, maana yake ndani yako kuna hisia kuwa hajatulia. Ni malaya au kicheche kwa lugha ya mtaani.Je, unadhani ni vema kumuona mwenzi wako hajatulia? Kama ndivyo, unaendelea kuwa naye kwa sababu gani? Asipoheshimiwa na wewe, unataka nani mwingine ampe heshima?Mwenzi wako anapogundua kuwa humheshimu, taratibu naye atakushusha thamani. Akigundua huna imani naye, atakosa raha. Hata kama anakustahi leo, ipo siku ataona hana sababu ya kuendelea na wewe.Mwingine anahaha kuulizia nyendo za mwenzi wake kwa marafiki. Hilo ni kosa kubwa kwa sababu huyo unayemuuliza, mwisho anaondoka na kitu kikubwa kwamba hakuna uaminifukwenye uhusiano wako.Kuna mtu ambaye huweka mabodigadi wa kufuatilia nyendo za mke wake kila anapokwenda. Anayedhani kufanya hivyo ni dawa, ameula wa chuya kwa uvivuwa kuchagua. Anakosea kupita kiasi.

Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out