Sunday 23 August 2015

Haya Ndio Anayoyapenda Mume Wangu na Kuiharibu Ndoa Yangu

Ndugu zangu,
Nilishawai kuwaambia hali ngumu ya mapenzi ninayoipitia ndani ya miaka miwili,kwa kifupi ni kuwa mwanaume unalalanae miezi 2 hajakugusa, ukimgusa anasema amechoka.

Juzi nilikuwa napitia Fb yake nimekuta amewa add wadada wa 4 hivi tofauti na katika wadada hao wote ni ambao mtu anaejiheshimu na mwenye busara hawezi kuwa add, ni watu wasio na maadili mema, picha zao zimekaa kikujiuza, na ata ukiangalia friends wao hao kina dada ni wanaume zaidi ya 600.

Wanawake unaweza kuta wa4 tu, mr. uwa anasafiri sana kikazi anaenda jiji flani hapahapa TZ na hao aliowa add wanapatikana jiji hilohilo nikiangalia profile zao, naanza kuamini kuwa hii hali ngumu ya mapenzi ninayopitia anaisababisha yeye kwa makusudi na wala sio shetani bali anaudekeza moyo wake unachoona.

Hivohivo, sijamuuliza na sitomuuliza naona tabu kumuuliza maana nishalalamika sana lakini sioni mabadiliko, sio wanaume wote wanaosafiri kikazi wanaendea kazi wengine wanaendea ufuska tu.Nilijaribu kwenda katika fb page nikaingiza namba yake nimekuta ana account nyingine nayo haieleweki.

Kaiita kama majina kama vile (Zanzibarbongo) sio jina halisi, hapa mnielewe namaanisha hivi namba ya simu ukiisajili katika kufungulia account ya fb inaonesha hiyo account, so baada ya kuweka namba yake nimekutana na hiyo account it means kwamba ya kwake, wakati huohuo ana account ambayo inafahamika,

Najiuliza anatafuta nini? Mke wake mie msichana tu, najimudu, nafanya kazi mzuri, nina umbo zuri, na kazi zote nifanyazo lazima nihakikishe napika chakula cha usiku kwa mkono wangu, na mengine yote ya kumfanyia mume namfanyia, jamani huyu mwanaume asieridhika na alichonacho anatafuta nini?

All in all nimechoka na hii hali na siku zinavoenda mapenzi yanaisha kabisa kwake.

Nifanye nini ndugu zangu?