Wednesday 22 July 2015

Ushauri: Mume Hataki Kufanya Mapenzi na Mimi, Anamtaka Mtoto Niliyezaa Kabla ya Kunioa


Naombeni ushauri wenu, 
Mawazo ya wengi ndio nitakayoyafanyia 
kazi. Nimefunga ndoa na mwanaume 
mwenye watoto 4 wawili wakike wawali 
wa kiume. Mama yao alifariki kwa ajali ya 
gari aliwaacha wadogo wakiwa primary. 
Na mimi niliolewa nikiwa na mtoto 
mmoja wa kike ambae kiumri 
analongana na mtoto wake watatu. 
Kusema ukweli mwanzoni iliniwia 
ngumu sana kukubali ombi lake hasa 
nikifikiria kulea watoto wa mama 
mwingine wanikubali, je, vipi kuhusu 
huyu nilienae? 
Baada ya muda kupita na kukolea 
kimapenzi nilijubaliana nae tukafunga 
ndoa tukaunganisha familia wote 
wakawa kitu kimoja. Mungu akabariki 
tujaliwa kupata mtoto mmoja. Kiukweli 
niliwapenda sana hawa watoto, 
niliwalea kama wangu. 
Nilijitahidi kadri ya uwezo wangu 
kuwafanya wasijione wakiwa. Kama 
zawadi nk nilitowa mezani bila kubagua 
sikupenda kuweka makundi na hili 
shahidi ni Mungu pekee. Watoto watatu 
wapo chuo kikuu na mmoja wa kwake 
yupo form six. 
Katika ndoa yangu kulikua na 
migongano upande wa tendo la ndoa, 
kabla ya ndoa tukiwa kwenye stori za 
mapenzi niliwahi kumweleza 
mwenzangu kuwa mimi sio mtundu 
sana upande wa sex ivyo ningependa 
yeye awe mwalimu kwangu kwani 
tangu mwanaume wa kwanza 
anidanganye na kunipa ujauzito sikuwa 
tena kuwa na byfriend. 
Akiniambia sawa. Tulipoingia kwenye 
ndoa mwenzangu alianza kubadilika 
wakati mwingine alikaa hata miez 8-10 
bila kutaka sex.Nikimuuliza husema 
amechoka au hajisikii. 
Hata huo muda anaokaa mpaka mimi 
nimchokoze na hii nikutakana na 
kushindwa kuvumilia. Kuna wakat 
aliamua kuniambia ukweli kuwa sijui 
mapenzi, niliumia ila nilikubali kuwa ni 
kweli sijui ila anisaidie kujua. 
Hakufanya ivo. Ilifikiwa wakati nikaona 
ngoja nikae nisimsumbue ila nilijiuliza 
nitaishi hivi mpaka lini na kusaliti ndoa 
siwezi. Nilimwomba Mungu sana anipe 
uvumilivu ila pia Mungu aseme na mimi 
juu ya hii ndoa. 
Mungu ni mwaminifu. Baada baada ya 
maombi ya zaidi ya mwaka mke wa 
shemeji yangu alileta malalamiko kuwa 
mume wangu amekua akimsubua sana 
kimapenzi ikiwa ni pamoja nakumtumia 
picha za ex. 
Niliziona hakuishia hapo akasema hata 
hawa wadada wa kazi huwa anatembea 
nao. Nilipowabana waliopo na 
walioondoka walikubali na kunipa 
ushahidi. Mbaya zaidi hata huyu 
mwanangu alishamtaka kimapenzi sina 
uhakika kama alifanikiwa au la. 
Ninaumia sana sana. Mtaani ndoa yangu 
imekua mfano wa kuigwa hio ni 
kutokana na jinsi tunavoonekana kwa 
watu. Lakini hii yote onatokana na jinsi 
nisivopenda watu wajue mambo ya 
ndani. Ninampenda, ninamheshim, 
ninamjali.Siruhusu nguo au chakula cha 
mume wangu afanye mwingine 
nikiwepo. 
Hata kama tumegombana nisingependa 
yoyote ajue, nilijitahidi sana, kuwa mtiifu 
na mnyenyekevu kwake. Hii nikutokana 
na malezi niliyolelewa. Hata kama 
amesafiri watoto watajua baba anarudi 
kwakua wataniona jinsi ninavokua busy 
jikoni na kuandaa juisi na matunda. 
Ushauri wenu muhimu sana kwangu 
Asanteni