Thursday 30 July 2015

HIZI NDIZO NJIA 10 ZINAZOTUMIWA NA WANAWAKE KUTONGOZA WANAUME

Nina uhakika mkubwa wewe kama mwanaume ushawahi kutongozwa na mwanamke bilakujitambua. Na pia nina uhakika mkubwa zaidi wewe kama mwanamke ushawahikumtongoza mwanaume kwa njia flani ambayo ulitaka usijulikane.

So kama wewe ni mwanaume au kamawewe ni mwanamke nimeamua kuumwaga mtamakueleza mbinu zote ambazo hutumiwa na wanawake kutongoza wanaume kwa njia yakisiri.

Ok. Kabla tuanze kuorodhesha njia hizi 10 ambazo wanawake hutumia kutongozawanaume, tunafaa kuelewa ya kwamba wanawake wanaamini kuwa mwanaume ni kiumbeambacho haelewi chochotekuhusu wanawake.

hata akitaka kujua kila kitu kuhusu mwanamke kile atakachopata ni asilimia 10% ya yoteambayo mwanamke anayojua so kuweka hii orodha hapa ni baadhi tu ya njia ambazowanawake hutumia.

Njia zenyewe ndizo hizi (Psss! wanawake jaribuni kutumia hizi mbinu kama kunamwanaume unayemzia na haonyeshi dalili za mshiko kwako..

1. Kuikunja miguu

Wanawake hutumia mbinu ya kuikunja miguu yao kimtindo ambapo wanajaribu kuonyeshashepu ya mwili aka kiuno. Ukiona mwanamke anapenda sana kuikunja miguu yake pindiunapokuwa umekaa na yeye mnaongea ni moja wapo ya dalili.

2. Kupapasa na kurusha nywele zake
Hii ni mbinu ambayo hutumiwa sana na wanawake lakini mpaka sahizi wanaume wengihawajafahamu kama hii ni mbinu moja wapo wanawake hutumia kutongoza wanaume. Pia kama unataka kujua kuwa mwanamke anakutongoza angalia vile hairstyleyakeanavyoiweka.

Ukiona mwanamke kawaida nywele zake anazifanya zilale nyuma lakini maramoja amanyingine huweka baadhi ya nywele zake karibu na macho kama yuko na wewe basi fahamuhio ni mbinu anayoitumia kukutongoza

3. Kujipamba kila baada ya dakika tano
Ushawahi kuongea na mwanamke halafu baada ya dakika fulani anaomba ruhusa yakuenda msalani? Halafu inatokea mara kwamara tatizo ni hilo hilo la kuenda msalani kilaanapokuwa na wewe? Ushajiuliza ni kwanini? Owk acha nikufungue macho.

Mwanamke akikuomba ruhusa kuenda msalani huwa mara nyingi anaenda kujipodoambele ya kioo. Ukiwa makini utakuwa umegundua kila anapotoka msalani huwaanapendeza zaidi. Well, sijui anajipaka nini akiwa huko msalani lakini hio ni moja ya daliliya kuonyesha kuwa mwanamke anakutongoza.

4. Kufinya jicho
Wanaume wengine wanaweza kufinyiwa jicho na mwanamke bila wao kufahamu chochote.Ni wachache pekee ndio wanaweza kutambua hilo na kuchukua hatua ya pili. 
Hii pointi naona inajieleza yenyewe manake kufinyia mtu jichoinaonyesha kuwaumependezwa nakitu fulani na wala si kuwa umeingiwa na uchafu kwa jicho.

5. Kutabasamu na kuchekacheka
Wanawake wanatumia mbinu hii ili kumfanya mwanaume ajione kuwa yeye anaongea vituambavyo vinafurahisha. Kama unamjua mwanamke ambaye anapenda sana kuchekachochote unachoongea basi usipoteze nafasizaidi. Anza kampeni ya kumnasua awe wako namapema.

6. Kuleta wivu
Wanawake wengi hawapendi kuongea kuhusu mambo ya nyuma waliyoyapitia awali. Lakiniukikutana na mwanamke ambaye anafunguka moyo wake na kuanza kuelezea mamboyake, wapenzi wake wa zamani na jinsi anawachukia baadhi ya waname ujue ni dalili mojaya kukuonyesha kuwa amelike kampany yako. Ikifikahapa fanya fasta kabla hujapoteza.

7. Kupenda kukusifu
Ukiona unafanya jambo halafu baada ya hapo mwanamke anakusifia ujue amependezwana wewe. Hii inaweza kuwa vile ulivyovalia, mitindo yako ya maishaunayopenda kufanyaama chochote kile ukiona anapenda kukusifia ujue kuwa 'anataka kitu' kutoka kwako.

8. Whatsapp yako ama facebook yako haitoki
Mitandao ya kijamii ni moja wapo ya njia rahisi kwa mtu kujieleza ya moyo wake bilakujishuku hivyo ukiona mwanamke anakuapproach na kutaka stori kwa whatsapp amafacebook yako usimlenge. Chukua hatua ya haraka kuhakikisha kuwa unaongeza uhusianowake na wako

9. Kutafuna ubani ama ballgum
Owk hii nilikuwa nikiipinga mpaka nikaja kuuliza baadhi ya wanawake kuhusu utafunaji waubani kama ni mbinu moja wapo ya kutongoza na bila kupinga walikubali. Pia si mara ya kwanza kuambiwa na baadhi ya wanaume kuwa wanapenda vile wanawake wanavyotafunaubani.Utafunaji wa ubani humpa nafasi mwanamke kuondoa midomo yake vile anavyotakayeye hivyo imebainisha kuwa ni mbinu moja wapo ambayo huitumia kutongoza.

10. Kutuma jumbe za usiku mwema
Kama vile ilivyobainika na wanasayansi kuwa meseji inayotumiwa mtu wakati wa mwishokabla hajalala ndio mtu atakayemfikiria wakati anapoamka. Ni dhahiri kuwa kuna ukweliwake kiasi flani. Hivyo hivyo ukiona kuwa mwanamke anakutumia text wakatiwa usiku wakiza fahamu kuna kitu kiko jikoni.